Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imetiliana saini makabidhiano ya Chuo cha mafunzo ya Amali kiopo Daya kisiwani Pemba baada ya kukamilika rasmi.
Akizungumza baada
ya makabidhiano hayo Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
Zanzibar Dkt Idrissa Muslim Hija amesema kutokana na kukamilika kwa
ujenzi wa Chuo hicho ipo haja ya kuanza kutumika ili wananchi waweze
kunufaika katika kupata taaluma,
Ameeleza
kuwa matarajio yao ni kuanza kutoa Mafunzo ndani ya chuo hicho Februari
mwakani pamoja na chuo cha Amali kiopo Makunduchi Unguja.
Aidha
Dkt Idrissa ameutaka uongozi wa Mamlaka ya Mafunzo ya Amali kuweka
utaratibu maalumu na kuandaa mazingira kwa ajili ya Wanafunzi kuanza
kujiandikisha katika chuo hicho ili utakapofika Februari waweze kuanza
masomo yao.
Hata hivyo
Dkt Idrissa ameishukuru kampuni ya ZECCON kutoka Tanzania bara kwa
kuweza kukamilisha kazi hiyo kwa kiwango kinachoridhisha na kuwapongeza
wote walioshiriki kwa namna moja ama nyengine katika kuusimamia ujenzi
huo tokea ulivyoanza hadi kukabidhiwa.
Kwa
upande wake Mkandarasi wa ujenzi wa Chuo cha Amali Daya Bw Ali Mbarouk
Juma ameishukuru Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kwa
kumuamini na kuweza kumpatia kazi hiyo ambayo tayari imekamilika katika
kiwango kilicho takiwa.
Pia
ameeeleza kuwa atayafanyia kazi yale yote ambayo Wizara imemuomba
kuyakamilisha na kuahidi kuyakamilisha bila ya malipo yoyote, ikiwemo
ufungaji wa AC katika chumba maalum cha kompyuta, ikiwa ni ishara ya
uzalendo kwa nchi yake.
Naye
mshauri elekezi wa mradi huo Bw. Mohammed Suleiman Nassor ameipongeza
Wizara ya Elimu kwa mashirikiano makubwa waliyowapatia kwa kipindi chote
cha ujenzi wa chuo hicho ambapo wameahidi kuendelea kutoa ushirikiano
wao kadri watakapohitajika.
Makabidhiano
hayo yamefanyika baina ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali na
kampuni ya ZECCON kutoka Tanzania Bara kwa kushirikiana na mshauri
elekezi wa Mradi huo.
No comments:
Post a Comment