HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 22, 2020

CHUO CHA MAFUNZO YA AMALI KIOPO DAYA KUANZA KUTUMIKA FEBRUARI 2021

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imetiliana saini makabidhiano ya Chuo cha  mafunzo ya Amali kiopo Daya kisiwani Pemba baada ya kukamilika rasmi.


Akizungumza baada ya makabidhiano hayo Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Dkt Idrissa Muslim Hija amesema kutokana na kukamilika kwa ujenzi wa Chuo hicho ipo haja ya kuanza kutumika ili wananchi waweze kunufaika katika kupata taaluma, 

Ameeleza kuwa matarajio yao ni kuanza kutoa Mafunzo ndani ya chuo hicho Februari mwakani pamoja na chuo cha Amali kiopo Makunduchi Unguja.


Aidha Dkt Idrissa ameutaka uongozi wa Mamlaka ya Mafunzo ya Amali kuweka utaratibu maalumu na kuandaa mazingira  kwa ajili ya Wanafunzi kuanza kujiandikisha katika chuo hicho ili utakapofika Februari  waweze kuanza masomo yao.

Hata hivyo Dkt Idrissa ameishukuru kampuni ya ZECCON kutoka Tanzania bara kwa kuweza kukamilisha kazi hiyo kwa kiwango kinachoridhisha na kuwapongeza wote walioshiriki kwa namna moja ama nyengine katika kuusimamia ujenzi huo tokea ulivyoanza hadi kukabidhiwa.

Kwa upande wake Mkandarasi wa ujenzi wa Chuo cha Amali Daya Bw Ali Mbarouk Juma ameishukuru Wizara  ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kwa kumuamini na kuweza kumpatia kazi hiyo ambayo tayari imekamilika katika kiwango kilicho takiwa.

Pia ameeeleza kuwa atayafanyia kazi yale yote ambayo Wizara imemuomba kuyakamilisha na kuahidi kuyakamilisha bila ya malipo yoyote, ikiwemo ufungaji wa AC  katika chumba maalum cha kompyuta, ikiwa ni ishara ya uzalendo kwa nchi yake.

Naye mshauri elekezi wa mradi huo  Bw. Mohammed Suleiman Nassor ameipongeza Wizara ya Elimu kwa mashirikiano makubwa waliyowapatia kwa kipindi chote cha ujenzi wa chuo hicho ambapo wameahidi kuendelea kutoa ushirikiano wao kadri watakapohitajika.

Makabidhiano hayo yamefanyika baina ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali na kampuni ya ZECCON kutoka Tanzania Bara kwa kushirikiana na mshauri elekezi wa Mradi huo.

No comments:

Post a Comment

Pages