Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto), akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) mkoa wa Mwanza katika kikao cha pamoja juu ya mikakati ya kuwasambaza Nishati hiyo katika maeneo ambayo hayajafikiwa. (Picha na Mpiga Picha Wetu).
NA MWANDISHI WETU, MWANZA
WAZIRI
wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,ametoa miezi mitatu kwa watendaji wa
Shirika la Umeme nchini (TANESCO) na Wakala wa Umeme Vijijini (REA),
kuhakikisha wanawaunganishia umeme wateja wote waliolipia ndani ya
miezi mitatu.
Waziri
Kalemani ameyasema hayo leo jijini MWANZA wakati akizungumza na
wafanyakazi wa TANESCO na REA katika kikao kazi cha pamoja
Amesema
ni lazima wateja wote walioko katika maeneo ya vijijini na kando kando
ya miji, wanaunganishiwa umeme kwa gharama ya Sh. 27,000 bila kujali
umbali wa mita 30 kwa kuwa ni wajibu wa TANESCO kuwafikishia wananchi
nguzo za umeme ili kuwafikia wateja hao.
"Mnataka
kila mwananchi awe mita 30 ndipo muwafikishie umeme? ni kazi yenu
kupeleka nguzo hadi muwafikie wananchi hao na nimeambiwa mnasubiri
sekula hii sasa ndiyo sekula nawapa ndani ya miezi mitatu nihakikishe
wateja wote wanaunganishiwa umeme"Amesema Dk.Kalemani
Dk
Kalemani pia ameitaka TANESCO kuanzisha madawati ya huduma kwa wateja
ili kuhakikisha wateja wanapatiwa huduma bora na kwa wakati ili
kuwaondolea adha wananchi ya kufuatilia maombi ya kuunganishiwa umeme
kwenye Ofisi za TANESCO Wilayani.
hata
hivyo Dk Kalemani amewataka watendaji wa TANESCO kuwafuata wateja
mahali walipo na kuepuka kutumia lugha ya kukatisha tamaa kwa wateja ili
kujenga mahusiano mazuri na wateja jambo litakalopelekea kupanua wigo
wa wateja na kuongeza mapato kwa Shirika.
Aidha,
Dkt. Kalemani, amewapongeza watumishi wa TANESCO kwa utendaji mzuri na
kueleza kuwa kwa zaidi ya asilimia 80 utendaji wa TANESCO ni wa
Kuridhisha.
Waziri
Kalemani amesifu utendaji mzuri wa Meneja wa TANESCO Kanda ya Ziwa
Mhandisi Henryfried Byabato na kueleza kuwa utendaji mzuri wa kazi
katika maeneo mengi aliyofanya kazi ndiyo uliopelekea Mha. Byabato
kupandishwa cheo.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika kikao kazi hicho, Naibu Waziri wa Nishati
Byabato, amewataka watumishi wote kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na
Waziri Kalemani, na atahakikisha anasimamia na kufuatilia utekelezaji
wake kwa ukamilifu.
Kikao
kazi baina ya Waziri Kalemani na watumishi wa TANESCO na REA, ni kikao
kazi cha pili baada ya kikao na wafanyakazi wa Mkoa wa Geita wiki moja
iliyopita. Lengo la vikao hivyo ni kuweka misingi ya pamoja ya utendaji
kazi unaolenga kuleta matokeo chanya na ya haraka katika Sekta ya
Nishati.
No comments:
Post a Comment