December 08, 2020

GREENWASTE YABULUZWA CMA

Na Mwandishi Wetu

WALIOKUA wafanyakazi wa Kampuni ya kuzoa taka Jiji la Dar as Salaam, GreenWaste Pro Limited wameiburiza kampuni hiyo katika Baraza la Usuluhishi na Uamuzi(CMA) ili kudai malipo na fidia ya kuachishwa kazi kinyume na mikataba yao.

Shauri hilo lilifanyika leo katika Baraza hilo chini ya msuluhishi Mpulla ambapo wafanyakazi hao wamedai kuwa, Januari 12,2020 kampuni hiyo iliwakamata wafanyakazi hao ambao ni 13, na kuwapeleka polisi kwa madai ya wizi wa fedha za kampuni huku akisitisha mikataba ya ajira bila ya kufuata utaratibu wa kisheria.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyazi hao, Sharif's Magombeka alidài kuwa wakati wanakamatwa alikua hawajapewa taarifa yoyote ya kuonyeshs wameachishwa kazi.

Alidai kuwa, katika kipindi hicho, yeye na wenzake waliwekwa mahabusu kwa siku kadhaa na kwa sababu alikua mjamzito wazazi wake walilazimika kumtafutia dhamana ili waweze kumtoa kwa kuwa siku za kujifungua zilikaribia.

Alidai Kuwa upelelezi wa shauri hilo ulichelewa hali iliyosababisha kushindwa kuwasilisha shauri hilo kwenye baraza hilo kwa wakati.

Aliiomba baraza hilo kusikiliza madai yao na kuyatolea uamuzi ili haki itendeke kutokana na kutolipwa haki zao katika kipindi chote walichokua wanafanyakazi.

Hata hivyo, Wakili wa Kampuni hiyo, Evans Ignas alidai kuwa hoja zilizowasilishwa na wafanyakazi hao ni batili kwa madai kuwa wanaweza kufungua shauri kwenye barazs hilo hata kama upelelezi unaendelea.

Alidai kuwa, wafanyakazi hao waliondewa kazini kwa kufuata taratibu za kisheria na kuliomba baraza hilo kutupilia mbali maombi hayo.

Hata hivyo, Msuluhishi aliahidi kutoa uamuzi mdogo ifikapo Desemba 18,2020 la kufungua shauri hilo nje ya muda.

No comments:

Post a Comment

Pages