December 08, 2020

TAMWA-ZANZIBAR WAJADILI MPANGO KAZI WA MWAKA 2021


Mkurugenzi wa TAMWA-Zanzibar Dkt,Mzuri Issa Ally akizungumza katika mkutano wa kujadili utendaji kazi wa shughuli mbalimbali za chama hicho katika kipindi kizima cha mwaka 2020 sambamba na kujadili mpango kazi wa mwaka 2021. 


Baadhi ya Wafanyaakazi wa TAMWA-Zanzibar wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa ripoti za kiutendaji katika kipindi cha mwkaa mzima wa 2020. 

 

 Na Talib Ussi, Zanzibar 


Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA-Zanzibar Dkt, Mzuri Issa Ally amewataka wafanyakazi wa taasisi hio kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza ufanisi kwa maslahi ya jamii yote.

 

Dkt, Mzuri aliyasema hayo katika hotel ya Ngalawa iliyopo shehia ya Bububu Kihinani nje kidogo ya mji wa Unguja  wakati alipokua akizungumza na wafanyakazi hao katika mkutano maalumu wa kujadili utendaji kazi katika kipindi cha mwaka mzima 2020 sambamba na kupanga mpango kazi wa mwaka 2021.

 

Alieleza kuwa kuna chanagamoto mbali mbali ndani ya jamii ambazo wananchi wanahitaji kuungwa mkono hivyo wafanyakazi wanapaswa kufahamu kuwa wanawajibu mkubwa kwa jamii.

 

‘’Kumekuepo kwa matukio mbali mbali ya udhalilishaji kwa kijinsia kwa wanawake na watoto pamoja na chanagmoto nyengine sasa ni wajibu wetu wafanyakazi kupingana na haya ikiwemo kutoa elimu zaidi na kuwawezesha wahanga kutoa ushahidi’’alisisitiza.

 

Katika hatua nyengine alisema licha ya uwepo wa kazi nyingi za kiutendaji katika kipindi  cha mwaka mzima2020 lakini wafanyakazi hawakuchoka na walifanya kazi kwa weledi mkubwa zaidi na yapo mafanikio ambayo yamepatikana .

 

Wakati hayo yakijiri Mkurugenzi huyo amewataka wafanayakazi hao kuhakikisha wanaongeza bidii na ufanisi mkubwa katika kazi zao kwenye kipindi  kinachofuata cha  mwaka 2021.

 

Awali akifungua mkutano huo Mjumbe wa bodi ya TAMWA-Zanzibar Bi Shifaa Said Hassan amewataka wafanayakazi hao kujikita pia katika kujiongeza kielimu wakiamiani kuwa elimu huongeza ufanisi kazini.

 

Pia aliwataka wafanayakazi kujitafakari kwa kila jambo kwenye utendaji na kuzifanya  chanagmoto kuwa sehemu ya marekebisho katika kipindi cha mwaka 2021.

 

Aidha aliwataka wafanyakazi kutoka tamaa na changamoto wanazokabiliana nazo na wazichukue changamoto hizo kuwa za kawaida kazini.

 

Miongoni mwa ripoti za kiuendaji zinazojadiliwa ni pamoja na matukio mbali mbali ya udhalilishaji,uwezeshaji wanawake kiuchumi na mengineyo.

No comments:

Post a Comment

Pages