December 30, 2020

KANISA LAWAKUMBUKA WAHITAJI

NA DANSON KAIJAGE, DODOMA


KANISA la TAG Upendo Revival Christian Center Dodoma imeazimisha siku ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo kwa kushiriki chakula cha mchana na wajane,yatima na watoto wanaotoka katika mazingira magumu.

Mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Dk Salum Vangasiti akizungumza na waumini waliokuwepo katika ibada ya maalum kushiriki chakula cha pamoja na yatima ,wajane na wale wanaotoka katika familia zenye uhitaji.

Mchungaji huyo amesema ni muhimu kushirikiana na makundi mbalimbali hususani katika siku muhimu kama kumbukizi ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo au mwakampa ili jamii hiyo nayo ijione kuwa ni sehemu ya furaha.

Mchungaji Dk.Salum amesema kanisa linawajibu wa kuhakikisha linafanya kazi kubwa katika jamii ambayo ni ya kuokoa roho za watu na kuhakikisha wanabarikiwa na kimwili.

"Kanisa letu limeona kuwa ni vyema siku kama ya leo ya kukumbuka kuzaliwa kwa Yesu Kristo ni vyema kufanya ibada ya kushirikiana na makundi mbalimbali ya watu wasiojiweza,yatima na wajane.

" Yesu Kristo anasema kuwa ibada iliyo njema ni pamoja na kuwajali watu wenye uhitaji kama tulivyofanya sisi licha ya kushirikia nao chakula cha pamoja bila kujali itikaji za dini pia tunatoa zawadi mbalimbali zikiwemo fedha"amesema Mchungaji Dk.Salum.

Akizungumzia habari ya amani ya nchi amewakata viongozi wote wa kisiasa,kidini pamoja na taasisi mbalimbali kufanya kazi zao kwa uadilifu sambamba na kutoa haki kwa kila mmoja.

"Ili uweze kuwa viongozi mzuri ni lazima ufanye kazi kwa misingi ya utii wa Kimungu pamoja na kujiondoa katika masuala ambayo yanaweza kukunyima ujasiri wa kutoa maamuzi.

" Kiongozi ambaye hatendi haki wala atoe maamuzi ya haki kamwe hawezi kujisimamia na hawezi kuwa na ujasiri wa kutoa haki kwa wale ambao wanaonewa"amesisitiza Mchungaji.Dk.Salum.

Akizungumzia viongozi wa kisiasa amewataka kuhakikisha wanatunza amani ya nchi pamoja na kufanya kazi kwa masilahi mapana kwa taifa na wananchi wake.


No comments:

Post a Comment

Pages