December 30, 2020

WATEJA 40 WA NMB WAIBUKA WASHINDI SHINDANO LA MASTABATA

Meneja Kitengo cha Kadi toka Benki ya NMB, Saidi Kiwanga akizungumza na waandishi wa habari (hapo pichani) jijini Dar es Salaam wakati wa kuendeshwa droo ya kuwapata washindi 40 katika shindano la ‘MastaBata Siyo Kikawaida’ linaloendeshwa na Benki hiyo ikiwa ni kuhamasisha matumizi ya kadi za Mastercard na Mastacard QR kufanya manunuzi ya bidhaa sehemu mbalimbali au huduma kupitia mtandaoni. Kushoto ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Bahati Nasibu Tanzania, Elibariki Sengasenga akisimamia zoezi hilo.
Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Bahati Nasibu Tanzania, Elibariki Sengasenga akifafanua jambo kwa wanahabari (hapo pichani) jijini Dar es Salaam wakati wa kuendeshwa droo ya kuwapata washindi 40 katika shindano la ‘MastaBata Siyo Kikawaida’ linaloendeshwa na Benki ya NMB ikiwa ni kuhamasisha matumizi ya kadi za Mastercard na Mastacard QR kufanya manunuzi ya bidhaa sehemu mbalimbali au huduma kupitia mtandaoni. Katikati ni Meneja Kitengo cha Kadi toka Benki ya NMB, Saidi Kiwanga, pamoja na Mtaalam wa Kadi kutoka NMB, Abeid Ng'anakilala wakifuatilia.

Meneja Kitengo cha Kadi toka Benki ya NMB, Saidi Kiwanga (kulia) akizungumza na mmoja wa washindi 40 katika shindano la ‘MastaBata Siyo Kikawaida’ kwa njia ya simu wakati wa droo hiyo. Kushoto ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Bahati Nasibu Tanzania, Elibariki Sengasenga akisimamia zoezi hilo.

Meneja Kitengo cha Kadi toka Benki ya NMB, Saidi Kiwanga (kulia) akizungumza na mmoja wa washindi 40 katika shindano la ‘MastaBata Siyo Kikawaida’ kwa njia ya simu wakati wa droo hiyo. Kushoto ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Bahati Nasibu Tanzania, Elibariki Sengasenga akisimamia zoezi hilo.


JUMLA YA WATEJA 40
 wa Benki ya NMB wameibuka washindi katika shindano la ‘MastaBata Siyo Kikawaida’ linaloendeshwa na Benki hiyo ikiwa ni kuhamasisha matumizi ya kadi za Mastercard na Mastacard QR kufanya manunuzi ya bidhaa sehemu mbalimbali au huduma kupitia mtandaoni. Washindi hao wametangazwa leo baada ya kujishindia fedha taslimu shilingi 100,000/- kila mmoja.

Akizungumza katika droo hiyo ya kuwapata washindi iliyoendeshwa Makao Makuu ya Benki ya NMB, jijini Dar es Salaam, Meneja Kitengo cha Kadi toka Benki hiyo, Saidi Kiwanga amesema wateja walioshinda leo ni 40 waliopatikana baada ya kuchezeshwa droo iliyosimamia na Bodi ya Michezo ya Bahati Nasibu Tanzania.

Alisema wateja hao tayari wamepigiwa simu na kujulishwa ushindi wao na fedha walizojishindia zitaingizwa moja kwa moja kwenye akaunti zao ndani ya saa 24 tangu kujulishwa ushindi wao. Akifafanua zaidi, Bw. Kiwanga alisema washindi hao wamepatikana kupitia kampeni ya ‘MastaBata Siyo Kikawaida’ inayoendeshwa kuhamasisha matumizi ya kadi za Mastercard na Mastacard QR kufanya manunuzi ya bidhaa sehemu mbalimbali au huduma kupitia mtandaoni.

Aidha alihamasisha wateja wa Benki ya NMB kuendelea kufanya manunuzi na malipo kwa kutumia kadi za Mastercard na Mastacard QR kwa bidhaa sehemu mbalimbali au huduma kupitia mtandaoni ili kuendelea kujishindia kwani zawadi badi zipo nyingi.

Hivi karibuni pia kupitia kampeni ya ‘MastaBata Siyo Kikawaida’ NMB iliwazawadia washindi 12 zawadi mbalimbali zikiwemo za simu janja, Runinga za kisasa, na Jokofu ambapo kila mshindi alipatiwa zawadi zenye thamani ya shilingi Milioni 2.4 kila mmoja. Promosheni hiyo ambayo ilizinduliwa Novemba, mwaka huu inatarajiwa kumalizika Februari, mwakani. 

Promosheni hiyo, inahamasisha utimiaji wa NMB Mastacard and Mastacard QR katika kufanya manunuzi bila ya kutumia pesa taslimu. Kila wiki na mwisho wa mwezi kuna droo zinafanyika na wateja kuendelea kishinda Zawadi mbalimbali. Wateja wanapaswa kufanya miamala yao kupitia kadi ya NMB Mastercard au QR mara nyingi wawezavyo ili kuongeza nafasi zaidi za kushinda. Katika kipindi chote cha kampeni, NMB itakabidhi zawadi kwa washindi 40 watakaoshinda Sh. 100,000 kila wiki na washindi 12 watazawadiwa simu janja aina ya Samsung galaxy Note20 yenye thamani ya Sh. milioni 2.4 kila mwezi.

No comments:

Post a Comment

Pages