December 06, 2020

WANAFUNZI WATAKAOFANYA VIZURI SHULE ZA KAIZILEGE NA KEMEBOZI KUSOMESHWA BURE

 Lydia Lugakila, Kagera

Katika kuongeza ushindani wa kitaaluma  taasisi za elimu za Kaizilege na Kemebozi zilizopo Bukoba mkoani Kagera zimeahidi kuwasomesha bure miaka miwili wanafunzi watakaoweza kuongoza kimasomo kitaifa kwa kushika nafasi ya kwanza  hadi ya tano.

Akieleza kauli hiyo  wakati akitoa taarifa ya shule za Kemebozi na Kaizilege katika mahafali ya kidato cha nne na darasa la saba Meneja wa shule hiyo Eurogius Katiti amesema kuwa mkurugenzi wa shule hiyo Eusto Kaizilege mwaka 2019 alianzisha tuzo maalum  ijulikanayo kwa jina la The Kaizilege excellence awards kwa wanafunzi watakaoweza kushika nafasi ya kwanza hadi ya tano na wale watakaoweza kufaulu vizuri kidato Cha 2 watasoma bure  kidato Cha 3 na Cha 4 bure huku watakao faulu kidato cha 5 na 6 kusoma bure.

Akielezea maendeleo ya shule hizo za Kaizilege na Kemebozi meneja huyo amesema kuwa shule hizo zimekuwa zikifanya vizuri na kuwa Kati ya shule Bora kiwilaya kimkoa na taifa na ni shule ambazo zimepeperusha vyema bendera ya heshima katika eneo hilo na Mkoa wa kagera kwa ujumla kwa kuongoza katika nafasi ya 1 kwenye mtihani wa taifa Mara kadhaa ambapo kwa miaka 14 shule hizo zimefanikiwa kuchukua tuzo ya Rais kwa kushirikiana na Elimu Sayansi na teknolojia pamoja na Tamisemi katika utunzaji wa mazingira  na upandaji miti.

Amefafanua kuwa kwa mwaka 2020 shule hiyo kwa kidato cha 6 wamepata tuzo kwa kuwa namba 2 kitaifa huku walimu 6 katika shule hiyo kuibuka wa kwanza kitaifa katika masomo mbali mbali na kupewa tuzo na vyeti  kutoka wizara ya Elimu wa kushirikiana na Tamisemi ikiwa ni katika kutambua mchango wao kitaifa ambapo pia mwaka 2019 kidato cha 4 walipata nafasi 1 kitaifa na kuifanya shule kupata tuzo kwa ushindi huo.

Katiti ameipongeza serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Magufuli kwa kuimalisha mahusiano mazuri na kuweka mazingira Bora ya uwekezaji katika sekta binafsi nchini.

 Aidha amewataka wazazi kutumia likizo kuwahimiza wanafunzi kuudhuria ibada takatifu na kujiadhali na starehe wanapokuwa nyumbani.

Kwa upande wao wanafunzi wa kidato cha nne katika lisala yao wamemshukuru meneja wa shule hiyo kwa juhudi zake za kubuni mikakati mbali mbali za usomaji pamoja na kuwatia Jambo lililowapa ufaulu mzuri.

 Naye mgeni rasmi katika mahafali hayo yaliyoendana na miaka 14 ya kuanzishwa kwa taasisi ya Kaizilege na kuzaliwa taasisi mpya ya Kemebozi Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheli Tanzania KKKT Dayosisi ya Kaskazini Magaharibi Abdnego Kesho Mshahara ameipongeza shule hiyo kwa ushindi mfululizo ki wilaya na kimkoa na kuuweka mkoa wa Kagera katika ramani nzuri ya taifa na kuwataka wahitimu hao kuwa na nidhamu inayoleta ushindi na ufanisi zaidi.

Hata hivyo Askofu huyo amewapongeza viongozi wa shule hizo kwa utoaji Elimu bora na miundo mbinu mizuri inayochochea ufanisi huku akiipongeza serikali hapa nchini kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji na hasa katika sekta ya Elimu baada ya kufanikiwa pakubwa.

No comments:

Post a Comment

Pages