December 04, 2020

Wadau kuzindua Mapungufu ya Sheria Zinazohusu Udhalilishaji

Wadau wa ukatili wa kijinsia kesho Disemba 5, 23020 watazindua mapungufu yaliyomo kwenye sheria zinazohusiana na ukatili wa kijinsia ikiwa ni sehemu ya vuguvugu la kupinga ukatili wa kijinsia.

Kongamano hilo ni mfululizo wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia na litafanyika katika ukumbi wa Watu wenye ulemavu, Kikwajuni Weles, Zanzibar.

Wadau hao wakiwemo Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA), Jumuia wa Wanawake Wenye Ulemavu (JUWAUZA), Mtandao wa Kijinsia Zanzibar (ZGC) na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Zanzibar (TAMWA ZNZ) walipitia sheria saba zinazohusiana na masuala hayo na kukuta tofauti na kukizana jambo ambalo linapelekea kukwama kwa kesi hizo katika vyombo vya sheria ama kupata hukumu ndogo. 

Sheria hizo ni pamoja na sheria ya Adhabu No 7 ya mwaka 2018, sheria ushahidi no 9 ya 2017, sheria ya mtoto no 6 ya 2011, sheria ya elimu No 6 ya 1982 sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai No. 6 ya 2018, sheria ya Mahakama ya kadhi No 9, 2017, sheria ya kumlinda mwari na mjane No 4 ya 2005.

Kongamano hilo litatoa nafasi kwa washiriki kujadili mapendekezo na nini kifanyike katika hatua za kuboresha sheria na utendaji wa taasisi husika katika kupunguza wingu la ukatili wa kijinsia.

Vitendo vya ukatili wa kijinsia vinaendelea kushamiri na bado kwa mujibu wa takwimu watu wanaopata hukumu ni kidogo sana ambapo kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi zinaonyesha kuwa kuanzia Januari 2019 hadi Agosti mwaka huu, malalamiko 821 ya ubakaji na ulawiti
 yameripotiwa lakini ni kesi nne tu hadi sasa ndizo zilizopatiwa hatia, sawa na asilimia 0.73% .

Hali hiyo inaonesha mapungufu makubwa katika sheria pamoja na utekelekezaji wake ambapo hutoa mwanya kwa wabakaji kukimbia makosa yao na hivyo kuendeleza tabia hiyo ovu.

Maadhaimisho ya Siku 16 za kumpinga ukatili wa kijnsia hufanyika kila mwaka kuanzia tarehe 25 Novemba hadi tarehe 10 Desemba, siku ya kilele chake.

No comments:

Post a Comment

Pages