HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 15, 2021

NECTA yatangaza matokeo, asilimia 85 waliofanya mtihani kidato cha nne wafaulu

Katibu Mtendaji NECTA, Dk. Charles Msonde.

BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA) leo Januari 15, 2021 limetangaza matokeo ya mtihani wa darasa la nne, kidato cha pili na cha nne mwaka 2020 huku yakionyesha kuwa asilimia 85 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne wamefaulu.

Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji NECTA, Dk. Charles Msonde amesema katika mtihani wa kidato cha nne jumla ya watahiniwa wa shule na kujitegemea 490,213 wakiwemo wasichana 258,323 ndio waliosajiliwa kufanya mtihani huo.

Amesema watahiniwa wa shule 434,654 waliofanya mtihani huo, 373,958 wamefaulu katika madaraja mbalimbali.

Hata hivyo amesema katika upimaji wa darasa la nne jumla ya watahiniwa 1,828,268 ndio waliokuwa wamesajiliwa kufanya mtihani huo na kati ya hao wa 917,940 sawa asilimia 50.21, huku wavulana wakiwa 910,328 sawa na asilimia 49.79.

“Kati ya wanafunzi hao waliosajiliwa wanafunzi Milioni 1.4 ndio walifanikiwa kufanya mtihani huo huku wanafunzi 123, 864 sawa na asilimia 6.77 hawakufanikiwa kufanya mtihani huo wa darasa la nne,” amesema.

Amesema katika mtihani wa kidato cha pili jumla ya watahiniwa 646,200 ndio waliosajiliwa kufanya mtihani huo ambapo kati ya hao wasichana walikuwa 344,339 sawa na asilimia 53.29 huku wavulana wakiwa 301,861 sawa na asilimia 46.71.

No comments:

Post a Comment

Pages