NA DANSON KAIJAGE, MWANZA
Waziri
wa Nishati, Mhe. Dk Medard Kalemani, amewaagiza watendaji wa TANESCO na
REA, kuhakikisha wanawaunganishia umeme wateja wote waliolipia ankara
za umeme jijini Mwanza na maeneo ya vijijini ndani ya miezi mitatu
kuanzia mwishoni mwa mwaka jana.
Waziri
Kalemani ameyasema hayo, alipokuwa akizungumza na Wafanyakazi wa
Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
katika kikao kazi cha pamoja kilichofanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu
jijini Mwanza.
Waziri
Kalemani, amewaelekeza watendaji hao wa TANESCO kuhakikisha wateja wote
walioko katika maeneo ya vijijini na kando kando ya miji,
wanaunganishiwa umeme kwa gharama ya Shilingi 27,000 bila kujali umbali
wa mita 30 kwani ni wajibu wa TANESCO kuwafikishia wananchi nguzo za
umeme ili kuwafikia wateja hao.
"Mnataka
kila mwananchi awe mita 30 ndipo muwafikishie umeme? Ni kazi yenu
kupeleka nguzo hadi muwafikie wananchi hao. Nimeambiwa mnasubiri sekula
hii sasa ndiyo sekula na wapa. Ni sisikie mtu anaongelea suala la mita
30 amesema Kalemani."
Waziri
Kalemani, ameitaka TANESCO kuanzisha madawati ya huduma kwa wateja ili
kuhakikisha wateja wanapatiwa huduma bora na kwa wakati na kuwaondolea
adha ya kufuatilia maombi ya kuunganishiwa umeme kwenye Ofisi za
TANESCO Wilayani.
Amewataka
watendaji wa TANESCO kuwafuata wateja mahali walipo na kuepuka kutumia
lugha ya kukatisha tamaa kwa wateja ili kujenga mahusiano mazuri na
wateja jambo litakalopelekea kupanua wigo wa wateja na kuongeza mapato
kwa Shirika.
" Masurveyor
ndio wanaolalamikiwa sana kwa kutoa lugha zinazokatisha tamaa.
Ninawasihi mbadilike kuanzia sasa. Atakayebainika anatumia lugha mbaya
kwa mteja, huyo tutaachana nae na atachukuliwa hatua za kinidhamu.
Wateja wote wahudumiwe bila kubaguliwa. Tunataka wateja wote wapate umeme bila kubaguliwa. Amesema Dkt. Kalemani.
Aidha,
Dkt. Kalemani, amewapongeza watumishi wa TANESCO kwa utendaji mzuri na
kueleza kuwa kwa zaidi ya asilimia 80 utendaji wa TANESCO ni wa
Kuridhisha.
Waziri
Kalemani amesifu utendaji mzuri wa Meneja wa TANESCO Kanda ya Ziwa
Mhandisi Henryfried Byabato na kueleza kuwa utendaji mzuri wa kazi
katika maeneo mengi aliyofanya kazi ndiyo uliopelekea Mha. Byabato
kupandishwa cheo.
Waziri
Kalemani pia ameelekeza watumishi walioajiriwa kwa muda (Short Term
Employees - STE) wanaohusika na kazi za kuwapimia umeme wananchi
wanunuliwe pikipiki zitakazowawezesha kuwafikia wateja kwa urahisi.
Aidha,
ameagiza kuwa watumishi hao (STE) wanaofanya kazi vizuri na waliofanya
kazi kwa muda mrefu waombewe kibali cha ajira ya kudumu Utumishi kupitia
Wizara ya Nishati.
Waziri
Kalemani amesisitiza umuhimu wa kufanya kazi kwa kasi, ubunifu na kwa
usahihi na amewataka watumishi wa TANESCO na REA kujiepusha na vitendo
vya rushwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika kikao kazi hicho, Naibu Waziri Byabato,
amewataka watumishi wote kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na Waziri
Kalemani, na atahakikisha anasimamia na kufuatilia utekelezaji wake kwa
ukamilifu.
Kikao kazi
baina ya Waziri Kalemani na watumishi wa TANESCO na REA, ni kikao kazi
cha pili baada ya kikao na wafanyakazi wa Mkoa wa Geita wiki moja
iliyopita. Lengo la vikao hivyo ni kuweka misingi ya pamoja ya utendaji
kazi unaolenga kuleta matokeo chanya na ya haraka katika Sekta ya
Nishati.
No comments:
Post a Comment