NA DANSON KAIJAGE, DODOMA
WAZAZI na Walezi wameshauriwa kuwalea watoto wao katika maisha ya kiuadilifu ili kuweza kupata taifa lenye watumishi waaminifu.
Kauli hiyo imetolewa na Askofu mstaafu wa kabisa la EAGT New Jerusalem Ihumwa Robert Mangwelaha amuda mfupi baada ya kumalizika kwa ibada ya kuwaweka watoto wakfu iliyofanyika kanisani hapo.
Amesema ili nchi iweze kuwa na viongozi waadirifu ambao wanachukia wizi,dhuruma,uonenu kwa wengine,wala rushwa na mafisadi ni lazima kujenga misingi mizuri kwa watoto wadogo.
Katika Ibada hiyo Askofu Mangwelaha maarufu kwa jina la mbeo Swanu amesema wazazi na walezi wwngi wamekuwa mbali na watoto wao jambo ambalo linasababisha mmonyoko wa maadili.
"Tunafanya ibada ya kuwaweka watoto wetu wakfu ikiwa ni mwaka 2021 ikiwa ni ishara ya kuwakabidhi watoto hawa mikononi mwa Mungu,lakini ibada hii isiwafanye wazazi na walezi kuwaacha watoto awa bila kuwajengea miongozo sahihi ya hofu ya Mungu.
" Wapo wazazi ambao wamekuwa mbali sana na watoto wao jambo ambalo linapelekea familia nyingi kutopeza tamaduni za kitanzania kuwa na tabia ambayo haina utukufu mbele za wanadamu wala Mungu.
"Hatuwezi kuwa na watumishi wa serikali,Kidini na taasisi mbalimbali ambao watakuwa na maadili mazuri kama watoto kuanzia ngazi ya familia hawajalelewa katika misingi mizuri ya kumpendeza Mungu" amesema askofu Mangwelaha.
Akizungumzia suala la utunzaji wa mazingira Mchungaji huyo amewataka watanzania kuhakikisha wanatunza mazingira kwa kupanda miti na kutunza miti kwa wingi.
"Utunzaji wa mazingira ni maelekezo kutoka kwa Mungu maana imeandikwa kuwa baada ya kuumba kila kitu anatengeneza busitani na kuweka kila kitu na kumwambia Adamu aitunze" amesema Askofu.
Aidha amewataka watanzania kuhakikisha wanatumia mvua zinzoendelea kunyesha kwa kupanda mazao ambayo yanaendana na sehemu husika.
No comments:
Post a Comment