HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 28, 2021

AMANI ITAFUNGUA FURSA KWA WAWEKEZAJI ZANZIBAR

MAKAMU wa Kwanza wa  Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman amewataka Wazanzibar  kuendeleza amani iliopo  ili kufungua fursa kwa wawekezaji toka nchi tofauti   kuja kuwekeza nchini.

 

Mkamu alitoa kauli hiyo wilaya Mjini wakati akikamilisha ziara katika Kisiwa cha Unguja iliyoandaliwa na Chama cha ACT Wazalendo kwa madhumuni ya kuwaona viongozi wa wanachama ambao wanasumbuliwa magonjwa tofauti.

 

Alisema amani iliyopo Zanzibar ndio kichocheo pekee cha kukuwa kiuchumi kwani mahala ambapo panakuwepo vurugu ni ngumu wawekezaji kuwekeza na kueleza hali ya kiuchumi huzidi kushuka.

 

Alisema hivi sasa watu wengi hawana ajira kwa sababu wanategemea chombo kimoja tuu ambachi ni Serikali na kufafanuwa kuwa kama wawekezaji wataingia zanzibar kila mmoja ataweza kupata ajira.

 

“Kiukweli hivi Serikali imejaa na nafasi za ajira hamna kwa hiyo nikuombeni tuisimamie amani yetu ili iwe kishawishi kwa wale ambao wanataka kuja kuwekeza kwetu basi wafanye hivyo” alisema Makamu.

 

Alisema kuwa ni ukweli usioficchika wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba wamechoshwa na umasikini miongoni mwao.

 

“Zanzibar inahitaji fikra mpya zitakazowaunganisha wananchi na viongozi wao ili kuikwamua kiuchumi” alisema Othman.

 

Alitoa changamoto kuwa ili kukabiliana na hali hiyo ni vyema Viongozi wa taasisi mbali mbali za serikali na binafsi kushuka kwa wananchi ili kukabiliana na changamoto zao

 

Makamu amebainisha ndio maana Serikali ya awamu ya nane inayoongozwa na Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi imekuwa ikiwataka viongozi kutoka maofisini na kuwaendea wananchi kujua shida zao.

 

Alisema Zanzibar inahitaji kutoka ilipo ili isonge mbele kiuchumi  na ifike katika hatua inayostahiki bila kujali misimamo ya kisiasa.

 

“In sha Allah tutafanyakazi ili tuifikishe Zanzibar pahala pake panapostahiki kiuchumi kutokana na hadhi yake” alisema Makamu huyo.

 

Aidha kwa upande wa kutolewa ajira kwa njia za misimamo ya kisiasa Makamu alibainisha hali hiyo inaweza kuiharimu Serikali kwa kuchukuwa watu ambao hawana sifa na kushindwa kufikia malengo yake.

 

 “Serikali ya Umoja wa kitaifa imekuja kwa ajili ya kuondoa mambo mbali mbali ikiwemo ubaguzi katika nafasi za Ajira Zanzibar” alisema Makamu.

 

Alisema katika Serikali hii ya awamu ya nane haikubaliani na hali hiyo na kueleza  akioneka mtendaji anafanya shuhuli yeyote ya Serikali kwa misimamo ya kisiasa atachukuliwa hatuwa.

 

Makamu alitoa kauli hiyo baada ya Mmoja kati ya wagonjwa aliowatembelea kumlalamikia kuwa ana watoto wake wameshamaliza kusoma Shahada ya kwanza lakini wakiomba ajira huwaambiwa wao ni wapinzani.

No comments:

Post a Comment

Pages