April 30, 2021

Dk.Mcharo: Watoto wenye ugonjwa wa mifupa laini wawahishwe hospitali


NA ASHA MWAKYONDE


WAZAZI wametakiwa kuwa na utaratibu wa kuwapeleka watoto wao kwa madaktari bingwa wa mifupa ili kuweza kugundua ugonjwa wa mifupa laini pindi anapozaliwa.

Mifupa laini ni ugonjwa ambao unawapata watoto wenye umri wa kuzaliwa na  hata katika umri wa miaka 10 na kuendelea.

Akizungumza  katika mahojiano jijini Dar es Salaam leo Aprili 30, Daktari Bingwa Mbobezi wa Magonjwa ya Upasuaji Mifupa kwa Watoto kutoka Taasisi ya Mifupi Muhimbili (MOI),Dk. Bryson Mcharo amesema kwa sasa Watanzania hawawezi kuliepuka tatizo hilo.

Dk.Mcharo amesema kwa nchi ambazo zimeendelea akizaliwa mtoto anapelekwa kwa daktari bingwa wa mifupa wa watoto lengo ni kugundua tatizo  na kuanza kupatiwa matibabu mapema.

"Bahati nzuri kwa sasa Tanzania ina madaktari bingwa wa mifupa wa watoto. Ni vizuri wazazi wakaanza kumpeleka  mtoto kwa daktari wa mifupa pindi anapozaliwa hasa wanapoona dalili ambazo sio sahihi," anesema.

Amesema tatizo hilo lipo na kwamba lina athiri watoto, takwimu zinaonyesha kati ya watu 15,000 mmoja anazaliwa na ugonjwa wa mifupa laini.

Dk.Mcharo amesema kuwa katika taasisi hiyo kuna madaktari wabobezi na kwamba wapo baadhi ya watoto walifika wakiwa hawajaanza kutembea  baada ya kupatiwa huduma wanatembea.

" Watu ambao wanahusika na kutoa huduma za afya wanapo waona watoto hawa  hasa wale wakunga wanapowazalisha  kwani dalili nyingi zinaonekana mwanzoni wawashauri wazazi," amesema Dk. Mcharo.

No comments:

Post a Comment

Pages