Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb), amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bi. Devotha Mdachi ili kupisha uchunguzi wa madai ya ubadhirifu wa fedha pamoja na masuala ya kiutawala yanayohusu Rasilimali Watu katika ofisi yake.
Kufuatia hatua hiyo Mhe. Waziri amemteua Betrita James Lyimo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo hadi pale uchunguzi utakapokamilika.
Aidha, Dkt. Damas Ndumbaro ameielekeza Bodi ya Wakurugenzi ya TTB kuwasimamisha kazi watumishi wengine wanaohusika na tuhuma hizo kwa kuwa suala hilo lipo chini ya Mamlaka yao ili waweza kupisha uchunguzi dhidi ya madai yanayowakabili.
Hata hivyo, Waziri Dkt. Ndumbaro amesema maamuzi hayo hayahusiani na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Uteuzi huo unaanza rasmi leo tarehe 10 Aprili, 2021.
April 10, 2021
Home
Unlabelled
MKURUGENZI MKUU WA BODI YA UTALII TANZANIA (TTB) ASIMAMISHWA KAZI
MKURUGENZI MKUU WA BODI YA UTALII TANZANIA (TTB) ASIMAMISHWA KAZI
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment