HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 10, 2021

TAKUKURU DODOMA YATOA TAARIFA YA UTENDAJI KAZI


Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utendaji wao kwa robo  mwaka kuanzi mwezi ya Januari hadi Machi mwaka huu.

 

 NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA

 

TAASISI ya Kuzuiauzui na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU ) Mkoa wa Dodoma imekuwa ikipokea malalamiko mengi kutoka kwa waajiri au wastaafu wa makampuni pamoja na taasisi binafsi wakilalamikia makato yao kutowasilishwa  katika mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF) kwa wakati.

Hayo yamesemwa leo  na Mkuu wa Takukuru Mkoa Dodoma Sosthenes Kibwengo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utendaji wao kwa robo  mwaka kuanzi mwezi ya Januari hadi Machi,mwaka huu.

Amesema kuwa hivyo imekuwa ikiwalete a usumbufu mkubwa kila wanapofuatilia mafao yao stahiki ya kisheria pia  hilo ni kosa la ubadhirifu kinyume cha kifungu cha 28cha sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa (sura 329Marejeo 2019) .

Kibwengo amesema ufatiriaji wao umeonyesha kwamba ni kweli kuna baadhi ya waajiri hawawasilishi sehemu ya makato yote ambayo wanayopaswa na hivyo, kwa kushirikiana na NSSF Mkoa wa Dodoma.

Pia amesema kuwa wameweza kudhibiti jumla ya Shilingi Milioni 214,182,548  kutoka  kwa waajiri therlathini ambao pamoja  na kukata sehemu  ya mishahara ya waajiriwa wao walibaki na fedha hizo, kinyume na taratibu, bila kuziwasilisha (NSSF) pia amewaasa waajiri hao MKoa wa Dodoma kuzingatia matakwa  ya kisheria na kujiepusha  na vitendo hivyo.

" Ufuatiliaji wetu kwa njia ya udhibiti wa vitendo vya rushwa na uchunguzi wa vitendo tumeweza kuokoa na kudhibiti Jumla ya Shilingi 704,191,582, nyumbani moja, kiwanja kimoja zikiwa ni mali ambazo zilichepushwa kinyume na makusudio,malipo ya tozo za Halmashauri yaliokuwa mikononi mwa watendaji  malipo dhaifu yasio stahili,".


Na kuongeza kuwa"Fedha hizo zilikuwa zichepushwe; na makati ya watumishi  wa sekta  binafsi ambavyo hayakuwa yamewasilishwa kwenye mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii  NSSF," amesema Kibwengo.

Ameongeza kusema kuwa wamekamilisha uchunguzi wa majalada 18  na kufungua mashauri mapya kumi mahakamani ambayo yanahusu watu binafsi  na watumishi wa umma kuanzia ngazi ya wizara hadi mitaa, pia wamepokea jumla ya malalamiko 210 ambapo 108 ndio yamehusisha rushwa.

 Amesema  wamefanikiwa kuokoa  Shilingi Milioni 27,000,000 kati ya fedha ambazo zimeokolewa zimetokana na ufatiliaji wa miradi miwili  ya maji ambapo wamebaini malipo batili kufanywa kwa wakandarasi  wa miradi ya vijiji vya Goima wilayani Chemba na Mundemu wilayani Bahi ili hali kazi amabazo zimeainishwa hazikufanyika.

Aidha amesema ,ukaguzi maalumu ulifanywa na Mdhibiti na Mkuguzi  Mkuu wa Hesabu za (CAG) ulithibitisha mapungufu hayo na kueleza, pamoja na hatua nyingine, wakandarasi na wasimamizi wa miradi hiyo warejeshe fedha zilizolipwa kinyume na taratibu.

No comments:

Post a Comment

Pages