HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 19, 2021

Ujezi wa bomba la Mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania kuanzia wakati wowote

 NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA

WAZIRI wa Nishati Dkt Merdad Kalemani amesema kuwa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga unatarajia kuanza wakati wowote kuanzia 
sasa. 
Ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akipokea taarifa maalumu ya majadiliano  ya wataalamu kuhusu ujenzi wa mradi huo.

Aidha kutokana na  ujenzi huo imeundwa tume ya wataalamu watakao simamia mradi huo ili kuhakikisha unakamilika kwa wakati.

“Baada ya majadiliano ya muda mrefu  taklibani miaka mitatu ya wataalamu wetu, sasa tunatarajia kuanza ujenzi haraka sana, na hatutegemei ujenzi uende zaidi ya miaka mitatu, tunataka ukamilike kwa wakati,”amesema

Dk Kalemani amesema kutokana na ukubwa wa mradi ameamua kuunda tume maalumu ya kusimamia mradi huo kama ilivyo miradi mingine ili kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa na mradi unakamilika kwa wakati.

“Kwa leo nataka kuunda tume maalumu ya kusimamia mradi huu na kwa kuanzia  nitamteua Dk Asiad Ngutu kuwa mratibu wa mradi, na mratibu msaidizi wa mradi  atakuwa Issa  Nyan’gao,  lakini Katibu Mkuu na TPDC mtaendelea kuongeza watu wengine wa kusaidiana na hao,

“Niwaombe sana ambao nimewateua  huu ni kama msalaba tumewapa kazi kubwa tunataka mkasimamie ujenzi wa mradi huu unakamilika kwa wakati na mambo yote yanayohusu mradi mnayasimamia ipasavyo,”ameeleza

Dk Kalemani amesema hadi sasa tayari serikali ya Uganda na Tanzania zimetenga Sh. Bilioni 28.8 kama fidia kwaajili ya kuwalipa wananchi wa tanzania ambao mradi utapita katika maeneo yao.

“Naipongeza serikali yetu na ya Uganda kwa kukubali kutoa Fedha kwaajili ya fidia, na tayaru hatua hii imekamilika kilichobaki ni kuanza kulipwa fidia kwa wananchi ili wapishe mradi,

“Natoa rai kwa wananchi ambao watapitiwa na mradi huu kuendelea kutoa ushirikiano hasa baada ya kulipwa fidia zao waondoke katika maeneo hayo ili mradi huo uanze mara moja bila kikwazo chochote,”ameeleza

Waziri kalemani pia amewata watu watakaopewa jukumu la kutoa fidia kwa wananchi kuhakikisha wanakuwa makini ili kila Mwananchi anastahili kulipwa fidia apewe kwa wakati bila kusumbuliwa na kucheleweshewa.

Amesema katika hatua za awali yatajengwa makambi zaidi ya 16 pamoja na eneo la kulainisha na kuunganisha  vyuma hivyo baadhi ya wananchi watapisha maeneo haya na fidia watalipwa ili wakaanzishe makazi yao mahali pengine.

“Ujenzi wa mradi huu unatarajia kutoa ajira zaidi ya 10,000 na tumependekeza asilimia 80 za ajira hizo wapewe watanzania  kasoro kazi zile ambazo watanzania watakosa sifa na kutakuwa na ulazima wa kiajili mtu kutoka nje ya nchi,

“Hii ni fursa kwa watanzania kuhakikisha maeneo yote ambayo mradi huu utapita wananchi wanajitokeza kwa wingi kupata ajira za muda na moja kwa moja.

 Mradi huu ulisainia  Mei 16 mwaka 2017 na Rais wa Serikali ya awamu ya tano hayati Dh John Magufuli na mwenzake Rais WA uGANDA  Makisio ya ujenzi wa bomba la kilomita 1445 limepangwa kuwa na uwezo wa kupitisha mapipa 216,000 ya mafuta kwa siku.

No comments:

Post a Comment

Pages