Kijana Mzalendo Frank Festo ( kulia), akimkabidhi stika yenye ujumbe " Mimi Nasimama na Mama Samia Salim Awali mara baadaha ya uzinduzi wa stika hiyo.
Na Asha Mwakyonde
WATANZANIA wametakiwa kuendeleza umoja na mshikamano na kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan ili kuiendeleza Tanzania katika nyanja mbalimbali ikiwamo uchumi.
Hayo yamesemwa jana jijini Dar es Salaam na Rais wa Chuo cha Bahari (DM), Salim Awali wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Stika ili kumuunga mkono Rais Samia yenye ujumbe " Mimi Nasimama na Mama Samia Wewe Je?".
Akizungumzia mara baada ya kukabidhiwa Stika hiyo na kijana Mzalendo Frank Festo amesema uzinduzi wa Stika hizo ni endelevu na kwamba lengo ni kuhakikisha kila mtanzania anaunga jitihada zinazofanywa na Rais Samia.
Awali alisema Rais Samia ameanza kurekebisha baadhi ya taasisi za Umma lengo likiwa ni kuwakumbusha majukumu ya taasisi hizo.
" Sisi wasomi tunasimama pamoja na Rais wetu Mama Samai katika kumuunga mkono jitihada anazozifanya na kuendeleza aliyoachia na Hayati Rais John Magufuli, "alisema.
Akikabidhi Stika hiyo kijana Mzalendo Festo alisema kuwa lengo
" Stika hii itasambazwa nchi nzima kwa kutumia njia ya vyombo vya habari, mitandao ya kijamii, vyombo vya usafiri, kutembelea ofisi za Umma.binafisi, vyuo, pamoja na nyumba za ibada, " alisema Festo.
Aliongeza kuwa lengo ni kuhakikisha ujumbe huo unamfikia kila mtanzania popote alipo.
Mzalendo huyo alizishukuru kampuni za Fero Consumable Products na High Siy kwa kuwezeshwa kuzalisha kampeni hiyo kuanza kwa kishindo.
Festo aliwaomba wadau wengine kujitokeza ili Stika hiyo izalishwe kwa wengi na kumfikia kila mtanzania mwenye mapenzi na taifa.

Ujumbe mzuri
ReplyDelete