May 31, 2021

ACT yahimiza mshikamano

 Mjumbe  wa  Kamati Kuu ya  Chama  cha  ACT  Wazalendo ambae  pia  ni  Makamo  wa Kwanza  wa  Rais Zanzibar    Othman  Masoud  Othman  amewataka  wanachama wa chama  hicho  kushikamana  kwa pamoja  ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa.

 

Kauli hiyo  alitoa huko  shangani Mkokotoni Wilaya ya Kaskazini A Unguja wakati kikao cha kutambulishwa kwake kwa viongozi na wafuasi wa chama hicho.

 

 Alisema umoja na  mshikamano  uliomo  ndani  ya  chama hicho  ndio  uliokipa  nguvu  na  heshima  ndani  ya  Zanzibar  na Tanzania  kwa  ujumla.

“Wazee  wetu  walisema  umoja  ni  nguvu  na  utengano  ni  udhaifu na  ambapo mshikamano huo   ndio uliopelekea uimara wa chama  ”

 

Alieleza  kuwa  mshikamno uliopo  ndani  ya  Act Wazalendo  imepelekea  kuzuia  migogoro  na malumbano  ndani  ya  chama hicho.

 

“Kwa sababu  ya  mshikamano  wetu  tumekuwa  hatuyumbi  katika  kudai haki pamoja na  mamlaka  ya Zanzibar  ndani  ya  Tanzania  na  nje  ya Tanzania ”  alisema Othman.

 

Alifahamisha  kua  wanzanzibar  na  watanzania  wengi  wanaingia  katika chama  cha  Act  wazalendo  kwa  kile  alichokitaja  kuvutiwa  na mashirikiano, Juhudi  na  dhamira njema.

 

Aliwataka  wafuasi wa chama  hicho  kutoichezea dhana  waliyonayo kwani ndio   njia  pekee yakufikia  kule  waliko kusudia  kuongoza Zanzibar  na Tanzania kwa ujumla.

 

Aidha alisema ili  kuyaenzi  aliyoyaacha kiongozi  wetu marehemu  maalim  Seif  Sharif  Hamad ni  kuendeleza umoja na mshikamano alioupigania kwa miaka   mingi uhai wake na historia ya  nchi  ya  Zanzibar.

 

Mjumbe  huyo  wa  kamati  kuu alisema  kuwa  mshikamano  umewajenga  ari  wanachama na  kuweza  kushindana  na  watu  waliokuwa  na  nguvu  ya  dola na  kueleza  kuwa  chama  hicho  kinajivunia  rasilimali  watu.

 

Sambamba  na  hayo  alisema  chama  cha  Act  wazalendo  kimeingia  katika serikali ya  umoja  wa kitaifa  GNU kwa ya kuleta  umoja  na  mshikamano  bila  ya  kujali  madhila waliyopitia  kutokana na  nguvu  kubwa  walizotumia  watawala.

“Tunalopigania  tuendeshe  nchi  yetu  kistarabu pasina mtu  yoyote  kupata  madhara  wakati  wa uchaguzi  na baada  ya  uchaguzi kwani tuna haki ya  kuishi  kwa  amani  katika  nchi  yetu.”alisema.

Mapema makamo mwenye  kiti  wa chama  hicho  Juma  Duni  Haji  akimtambulisha kiongozi huyo  alimtaka kuyasimamia  yote aliyoyaacha maalim Seif ambayo  yana  maslahi  Zanzibar pamoja  na  chama  kwa  ujumla.

“leo  nakutambulisha  kwa viongozi  wa  mikoa  ninachokuomba sasa usikae  nyuma  tuanze  kazi  ya  kujenga  chama  na kupigania  haki za wazanzibar” alisema Babu Juma.

Alisema kuwa Mjumbe huyo awali alikuwa msaidizi Mkubwa wa maalim Seif sharif wakati wa Uhai wake hasa kwa upande wa sheria.

Kwa upande  wake  katibu  wa  habar  na  uenezi  wa chama  hicho  Salum Abdalla Bimani alisema nchi  hii inataka  demokrasia  ya  kweli  yenye  maelewane  ili  nchi  iweze  kuneemeka  kutokana mashirikiano anamini  Zanzibar  itarudi  kwenye  hadhi yake.

“Mshikamano  na  umoja  wetu  ndani  ya  Zanzibar  utapelekea  kupata viongozi ambao watachaguliwa na wananchi kwa maana kwamba Yule aliyeshinda  katika  uchaguzi  apewe haki  yake”alisema Bimani.

 Akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa Mkoa wa Kaskazini A Kichama  Ali Angali Ali kwa niaba ya wafuasi wa chama hicho alisema wakotayari kumpatia mashirikiano yale ambayo yatampatia nguvu katika kutekeleza majukumu yake kichama na kiserikali.

No comments:

Post a Comment

Pages