May 31, 2021

Taaasisi ya MOI ina uhitaji wa damu

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Dkt. Respicious Boniface.

 

NA ASHA MWAKYONDE. DAR ES SALAAM

MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Dkt. Respicious Boniface amesema taasisi hiyo inauhitaji mkubwa wa damu kutokana na asilimia 65 ya wagonjwa wanaopokelewa wanahitaji kufanyiwa upasuaji.

Haya aliyasema jijini Dar es Salaam juzi wakati wa maadhimisho ya siku ya Wauguzi yaliyofanywa na waungzi wa taasisi hiyo, alisema MOI ni taasisi ya ubongo na mifupa na ni ya ajali matibabu mengi yanahitaji upasuaji.

Mkurugenzi huyo alisema asilimia 65 ya wagonjwa wanaofika MOI wataingia katika chumba cha upasuaji  ambao ni mrefu na kwamba sio wa muda mfupi.

Alitolea mfano upasuaji wa kutoa  uvimbe kwenye ubongo upasuaji wake ni mrefu na unahitaji damu  na kwamba watu waliopata ajali wanatoka damu hivyo uhitaji ni mkubwa katika taasisi hiyo.

" Damu haitengenezwi hakuna kiwanda cha damu hivyo tunawaomba Watanzania kuja kuchangia damu. Na nyie waandishi kupitia taaluma yenu tunaomba muhamaisishe jamii kuchangia damu, " alisema Dkt.Boniface.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA)  Tawi la MOI, Mosee Moses alisema damu imekuwa ni changamoto kubwa kwao kwa kuwa wanaishi na wagonjwa  na kwambwa waliliona kuna sababu ya kuihamasisha jamii kuchangia damu kwa muda wa siku tatu.

Alisema kuwa katika chupa walizozipata 133 kiwango kikubwa kimetoka kwa wauguzi ikiwa ni ujmbe kwa jamii ili iweze kuelewa changamoto waliyonayo

" Ukiwa na lishe njema unakuwa na kiwango kizuri cha damu unasaidia mwenzako  na unakuwa uneokoa maisha yake kwani damu hutibiwa kwa damu,' alisema Moses.

Kwa upande wake Miss Tanzana 2020/ 2021, Rose Manfere alisema kikubwa zaidi katika maadhimisho hayo wameweza kuchangia damu na kuokoa maisha ya watu wengine.

" Leo nimejumuika na Wauguzi wa MOI kwenye maadhimisho haya ya siku ya Wauguzi duniani ikiwa tumeanza tangu Mei 26 hadi 28 ambapo tunaendelea kuadhimisha "alisema.

No comments:

Post a Comment

Pages