May 24, 2021

Jafo ateua waandishi wa habari, wasanii kuwa mabalozi wa mazingira

 NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA

WAZIRI wa Nchi ,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jafo  ameteua  Wajumbe 14 washauri pamoja na mabalozi 40 wa kampeni ya Mazingira yenye  lengo la kuhakikisha Tanzania inakuwa Nchi shindani Duniani katika  kutunza Mazingira.

 Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Tarehe 24 /5/2021 Waziri huyo amesema kampeni hiyo imekuja baada ya maeneo kama vile maziwa na bahari kiwango cha maji kimepanda kutokana na uchafuzi wa mazingira katika maeneo hayo.

Kampeni hii ya Mazingira kwa Mwaka huu itahusisha kila Idara,zikiwemo Taasisi, Mikoa pamoja na Wilaya, kata vijiji na Mitaaa,Viwanda migodi na maeneo mbalimbali wakiwemo wadau wa Usafi na itaungana na utoaji wa tuzo mbalimbali kwa Washindi wa uandishi wa Habari za Mazingira ," amesema Jafo.

Na kuongeza kusema "Washindi 152 wa tuzo hiyo watapata nafasi yakwenda kutaliii katika Mbuga ya wanyama ya Mwalimu Nyerere na niwambie waandishi wa habari safari hii kuna zawadi kabambe zitatolewa kutokana na siku hii ya mazingira",amesema


Amesema kampeni hiyo ya Mazingira yenye kaulimbiu isemayo Mazingira yangu,Tanzania yangu,nakupenda daima  itazinduliwa rasmin June 5 Mwaka huu siku ya Kilele Cha maadhhimisho ya siku ya Mazingira Duniani ambapo  mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais DK. Philip Mpango mkoani Dodoma huku akisema  kampeni hiyo itakuwa endelevu.


Aidha Wajumbe14  ambao aliwateua kushauri mwendo wa kampeni,uteuzi wa majaji ili kuhakikisha kampeni inapata mafanikio makubwa kuwa ni Seif Ally Seif Mkurugenzi wa Superdoll ambaye ni Mwenyekiti Andrew Komba ni Katibu anatoka Ofisi ya Makamu wa Rais, process Dosantos Silayo Kamishina wa TFS


"Nanatarajia kukutana na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayohusika na mazingira mnamo mei27 Jijini Dodoma kwa lengo lakuiwezesha kampeni hiyo," amesema .
 Mabalozi 40 aliowateua wakiwemo wasanii pamoja na Waandishi wa Habari akiwemo Msanii Diamond platnums na harmonize.

No comments:

Post a Comment

Pages