May 24, 2021

Wanawake wa kilsamu watakiwa kusambaza elimu ya dini yao

 


NA HAMIDA RAMADAHANI, DODOMA


JAMII ya Wanawake wa Kiislamu wameaswa kusoma elimu ya dini ya kiislamu na kumjua  Allah pamoja na kumcha Allah ili kutengeneza kizazi chenye maadili.

Rai hiyo imetolewa jijini Dodoma na mbunge viti Maalumu mkoa wa Tanga Bi Mwantum Zodo wakati wa uzinduzi wa jengo la kituo cha elimu ya watoto na madarasa ya kinamama lilojengwa na umoja wawanawake wa jumuiya ya bi Khadija Dodoma.

Amesema Ili kutimiza Malengo makubwa ya kuishi hapa duniani wanawake wa kiislamu hawana budi kuwa mfano Bora katika jamii kwani Wanawake ndio walezi wa familia.

 "Umuhimu wa wanawake kuwa na elimu itawasaidia kulea familia zao katika madili mazuri ya kumjua Allah na kutenda matendo mema katika maisha yao," amesema Zodo.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa kituo cha watoto yatima cha Al-haafidhu Islamic ophance center kondoa ukht Aisha Khalfan amewaomba wakinamama wakiislam ambao wamejaaliwa kusoma elimu ya dini ya kiislamu kwenda kuisambaza .

" Niwaombe wakinamama wate wa kislamu waliobahatika kupata elimu muende kuisambaza kwa kufundisha watu wengine ili nao waweze kuelimika na kumcha Mwenyezi Mungu," amesema .

Awali akisoma risala kwa mgeni rasmi mwalimu wa madarasa ya Mhijirina Rahma Iddi amebainisha changamoto zinazoikabili taasisi hiyo ya jumuiya ya Bi Khadija Dodoma .

Ametaja changamoto hiyo nipamoja na kukosa vyanzo malumu vya kuiingizia tasisi hiyo mapato na taasisi hiyo kujiendesha kwa kutegemea misaada kutoka kwa watu mbalimbali wanaoiunga jumuiya hiyo mkono.

No comments:

Post a Comment

Pages