May 21, 2021

Katibu Mkuu CCM Chongolo atoa maelekezo katika Wizara tatu

 

Na Hamida Ramadhani, Dodoma


KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Daniel Chongolo amekutana na waandishi wa habari huku akitoa maelekezo ya kuondoa vikwazo kwa wananchi katika Wizara tatu ambazo ni Wizara ya Ardhi Nyumaba na Maendeleo ya Makazi ,Kilimo na Wizara ya Nishati

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma Katibu Mkuu huyo  amesema hadi kufikia 2025 Chama Cha Mapinduzi iliahidi kutunza rasilimali za aridhi ikiwemo kutatua migogoro yote ya ardhi kwani migogoro hiyo ya ardhi imekuwa ikiwapotezea muda wananchi.

Aidha amesema Chama Cha Mapinduzi CCM kupitia ilani yake imeielekeza Serikali kuhakikisha wanatoa hati miliki Katia umiliki wa ardhi na kwakufanya hivyo utawasaidia wananchi kuwa na Usalama wa maeneo yao.

" Tumefanya tathimini na tumegundua kwamba mpaka sasa ni wananchi wachache wanaomiliki ardhi wengi umiliki wa ardhi hawana ," amesema Chongoro.

Pia amesema kwa Upande wa uthaminishaji na fidia Wizara utengeneze  mfuko wa fidia  utakao leta haki kwa wananchi ambapo amewataka Viongozi wote wa ngazi zote kuhakikisha wanatatua migogoro ya ardhi katika maeneo yote yalionekana kuwa na migogoro.

KWA UPANDE WA MABARAZA YA ARDHI

Amesema Mabaraza ya ardhi yapewe fursa ya kusikiliza nakutatua changamoto mbalimbali na kuachana na mfumo wa kutoa hukumu na badala yake wahahikishe wanatoa Suluhu ya migogoro hiyo.

Amesema katika suala Zima la upimaji wa ardhi wahahikishe wanapima maeneo Ili kuyapanga na kuondoa ukuaji holela wa miji usiopanga.

" Pia Wizara ya Aridhi Nyumba  na Maendeleo ya makazi  kuhakisha wanaandaa mfumo wa utambuzi  kwa maeneo yanayoonekana kukua kwa kasi ili kuepuka kuwa na miji usiopanga," amesema Chongoro.

WIZARA YA  KILIMO 
 
Amesema Kilimo ndio Wizara mama ambayo inabaeba Watu wengi asilimia 70 hadi 80 wapo wananchi wamejikita kwenye Kilimo.

" Sisi kama Chama tawala tumeiona tuishauri Serikali kwenye bajeti ya Mwaka 2021/2022 kuweka mkazo Kilimo cha umwagiliaji kwani kwasasa ndio kimbilio la wengi wakulima kutokana na mvua zisizo  eleweka," amesema 

Amesema ili kukuza maeneo ya uzalishaji hekta Milioni 1.2 zitengwe na kila mwaka watenge maeneo ya umwagiliaji na sikimu za zilizoazishwa kujenga zikamilike na kwakufanya hivyo wigo wa uzalishaji wa Kilimo utaonekana.
 
MBEGU

Amesema changamoto kubwa kwa wakulima ni upatikanaji wa Mbegu bora hivyo Sisi kama Chama tawala tunaishauri Serikali kuweka bajeti ya Utafiti wa Mbegu bora Ili kuwapa uhakika wa mazao yao wakulima .

Amezitaka Taasisi zote zinazoshughulika na masuala ya tafiti zijiekekeze na ziwezeshwe Ili ziweze kutoka Mbegu bora.

" Ili kuwakuza wakulima wetu tunaishauri Serikali kupitia bajeti hii ya kilimo inayotalijiwa kusomwa hivi karibuni Wizara ya kilimo ijikite katika kutoa mikopo yenyemanufaa kwa wakulima ikiwemo pembejeo," amesema.

WIZARA YA NISHATI

Amesema kupitia bajeti ya mwaka 2021/2022  Chama Cha Mapinduzi CCM kinaelekeza yafuatayo kuweka kipaumbele katika upatikanaji wa umeme sehemu zote.

Pia amesema Chama kimesokitishwa na wale wote waliokuwa na nia mbaya au ovu na kusababisha kwa siku ya tati mfurulizo Watu kukuosa huduma ya umeme kuanzia tarehe 17 mwezi wa 5 hadi tarehe 20 mwaka huu.

" Chama CCM kinaonya vikali kwa wale wote watendaji waliokuwa  na nia mbaya kwa wananchi,kwani wananchi Wamepata hasara kwa kitendo hicho cha kukuza umeme kwa muda wa siku tati," amesema .

Sambamba na hayo amesema Ili kuwa na Nishati ya kutosha Chama Cha Mapinduzi kinaelekeza miradi yote ya usafirishaji, usambazaji unatekeleza kwa haraka.

Pia amesema vijiji na vitongoji vote vilivyoachwa katika usambazaji  vipate umeme na umeme uwe wa gharama za chini.

MAFUTA NA GESI ASILIA

Amempongeza  Rais wa Awamu ya Sita Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake katika kuhakikisha Ujenzi wa bomba kubwa la Mafuta inafanyikia kutaka Hoima nchini Uganda mpaka Tanga nchini Tanzanaia.


No comments:

Post a Comment

Pages