Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe (Mwenye tai ya Bluu) Prof. Lughano Kusiluka, akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania Bw. Deodatus Balile wakati wakizunguka kukagua jengo la mabweni lililomalizika ujenzi. Wanaoonekana nyuma yao ni Wahariri wa vyombo mbalimbali vya Habari nchini.
Baadhi ya wahariri wakisikiliza kwa makini maelezo kuhusu ujenzi wa miundombinu iliyokamilika.Wahariri hao walikuwa wanashiriki kikao cha Jukwaa la Wahariri kilichofanyika mkoani Morogoro.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka akijibu baadhi ya hoja za wahariri wakati walipofanya ziara chuoni hapo.
Wahariri wakikagua mazingira ya eneo la ujenzi Chuo hapo.
Wahariri wakiwa katika picha ya kumbukumbu na uongozi wa Chuo wa Kikuu Mzumbe, baada ya kuhitimisha ziara yao chuoni hapo.
Profesa Kusiluka amebainisha mafanikio hayo mbele ya Wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali nchini kupitia Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), waliotembelea Chuo Kikuu Mzumbe, Kampasi Kuu ya Morogoro na kupata fusra ya kutembelea maendeleo ya ujenzi wa miundombinu iliyokamilika.
.
Profesa Kusiluka amefafanua kuwa Chuo Kikuu cha Mzumbe kimewekeza zaidi ya Bil 13 kutokana na fedha zilizotolewa na Serikali, katika ujenzi wa vyumba vya madarasa na mabweni ya wanafunzi wa chuo hicho.
Amefahamisha kuwa ujenzi huo unalenga kukabiliana na changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa ya kufundishia na mabweni ya kulala wanafunzi, ambao baadhi yao wanalazimika kutafuta makazi nje ya kampasi.
Vyumba vya kufundishia vilivyo katika miradi mipya ya miundombinu iliyokamilika ina uwezo wa kuhudumia wanafunzi 1,000 huku mabweni yakiwa na uwezo wa kutoa malazi kwa wanafunzi 1,024.
Aidha, amewashukuru Wahariri wa vyombo vya habari kwa kutenga muda wao kutembelea Chuo Kikuu cha Mzumbe, chuo ambacho kinajivunia mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuzalisha viongozi wengi ndani Serikali akiwemo Rais wa Awamu ya Sita Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Aidha Profesa Kusiluka amebanisha kuwa Vyombo vya Habari, Wahariri na Waandishi wa habari wana umuhimu mkubwa wa kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha jamii ikiwa ni pamoja na kuchochea maendeleo.
Wakizungumza baada ya kutembelea majengo yaliyokamilika (Vyumba vya madarasa na mabweni ya wanafunzi), wahariri hao wamepongeza mafaniko makubwa yaliyotokana na dhamira ya Serikali ya kuwekeza kwenye Sekta ya elimu ili kutoa fursa kwa Watanzania wengi zaidi kunufaika na Elimu nchini.
No comments:
Post a Comment