UMOJA wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) unaratajia kushiriki Maadhimisho ya Siku ya Makumbusho Duniani. Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa juzi Katibu Mkuu wa TAMUFO, Stella Joel alisema tayari wanamuziki kadhaa wameonesha nia ya kuadhimisha siku hiyo. " Baadhi ya wanamuziki wameonesha nia ya kuhudhuria maadhimisho hayo ya makumbusho ya Taifa yatakayofanyika Mei 18, 2021." alisema Joel. Mlezi wa TAMUFO, Frank Richard alisema muziki ni sehemu katika Kuadhimisha Siku ya Makumbusho Duniani. " Muziki ni wa muhimu sana hasa katika kipindi hiki ambacho tunahamasisha uanzishwaji wa makumbusho mbalimbali hapa nchini zikiwemo za Wanamuziki kama mataifa mengine yaliyoendelea yanavyofanya. Richard alisema nchi nyingi duniani zina makumbusho mbalimbali zikiwemo za wanamuziki hivyo umefika wakati kwa wanamuziki wa Tanzania kupata elimu kuhusu makumbusho ili waweze kuzianzisha chini ya taratibu na sheria za nchi. |
Katibu Mkuu wa TAMUFO, Stella Joel.
Na Dotto Mwaibale
No comments:
Post a Comment