HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 20, 2021

TASAC Yawajengea Uwezo Wahariri na Wanahabari Dar

Na Hussein Ndungulile,  Dar es Salaam
 
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) imeendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo wahariri na waandishi wa habari juu ya  shughuli zake na sheria zinazosimamia sekta ya majini.

Akiwasilisha mada katika semina hiyo Afisa Uhusiano wa TASAC, bw.Nicholaus Kinyariri  alisema  lengo la semina hii ni kuwajengea uelewa na uwezo wa jinsi ya kuripoti maswala yanayohusu sekta hiyo.

Amebainisha kuwa TASAC ipo chini ya wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na kwamba imeanzishwa chini ya kifungu namba 4 cha sheria 14 ya mwaka 2017 ambayo rasmi ilianza kutumika mwaka 2018.

"TASAC imeamua kutoa semina hii kutokana na kuwepo uelewa mdogo kwa jamii kuhusiana na shughuli zake na sheria mbalimbali zinazosimamia sekta ya majini, " Alisema bw. Nicholaus.

Alisema TASAC ina majukumu mbalimbali inayotekeleza yakiwemo ya usimamizi na udhibiti huduma za Bandari na usafiri wa Meli, Biashara ya Meli katika maeneo husika pamoja na kusimamia maslahi mapana ya bidhaa za kipekee wanzaopaswa kuzisimamia.

"TASAC pia imepewa jukumu la kusajili vyombo vya majini kuanzia mita nne,  vyombo vya Uvuvi na Starehe." Alisema.

Aliongeza kuwa tangu TASAC kuanzishwa kwake imeweza kupata mafanikio mbalimbali ikiwemo kuchangia gawio kwa serikali la Sh Bilioni 40, utoaji wa leseni 804 za Uwakala wa meli, kachangia mapato ya serikali pamoja na kuboresha huduma za usafiri wa majini.

Pia alibainisha kuwa shirika katika kutimiza majukumu yake wanashirikiana na wadau wengine wakiwemo mamlaka ya Mapato Tanzania {TRA), Jeshi la Polisi-kikosi cha Majini, Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini ( TMA).

Kwa upande wake Meneja Udhibiti wa huduma za Bandari bw. Julius Mitinje Alisema shirika hilo linafanya udhibiti katika maeneo ya mwambao wa bandari za Dar es salaam, Tanga na Mtwara pia kwa upande wa maziwa ni Ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa.

Alisema wamekuwa wakifanya uhakiki wa uzito wa mizigo ndani  ya makasha, Bandari kavu na watoa huduma mchanganyiko bandarini.

No comments:

Post a Comment

Pages