May 19, 2021

Tilioni 4 zatengwa miradi ya ujenzi



Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Malongo, akizungumza na wahandisi walioshiriki mafunzo ya usimamizi wa miradi wakati alipokuwa akifungua mafunzo hayo, jijini Dodoma.
 
 
 
NA HAMID RAMADHANI, DODOMA


KATIKA mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali imetenga jumla ya shilingi Tilioni 4 kwa ajili ya miradi ya Ujenzi ambayo umepangwa kutekelezwa hapa nchini.

Kutokana na hayo serikali  imewataka Wahandisi kuhakikisha  wanakamilisha miradi yote mikubwa ya kimkakati iliyoanzishwa na serikali ya awamu tano kwa lengo la kukuza uchumi na kujenga Tanzania ya viwanda.

Hayo yalibainishwa leo na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi(ujenzi)  Mhandisi Joseph Malongo wakati akifungua warsha ya siku tatu kwa wahandisi nakuitaja miradi hiyo kuwa ni Daraja la Salenda,Daraja la Busisi, Miradi wa kufua umeme na Reli ya kisasa

Amesema Serikali iliyopitia iliandaa miradi mikubwa ya kimkakati na serikali ya awamu ya sita imeahidi kutekeleza, waandisi mnajukumu kubwa la kuhakikisha miradi hii inakamilika kwa wakati kwasababu kukamilika kwake itakuwa ni chachu ya maendeleo kwa Taifa,

"Katika nchi hizi ambazo bado zinaendelea sekta ya ujenzi ni muhimu sana kwasababu inachangia asilimia kubwa ya maendeleo ya viwanda na biashara hivyo kuongeza ukuaji wa uchumi," alisema

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wahandisi Prof Ninatubu Lema amesema wamejipanga kuhakikisha wanashirikiana na serikali kukamilisha miradi yote mikubwa ambayo tayari ilishaanzishwa.

Amesema serikali imewapa jukumu hilo la utekelezaji wa miradi hiyo ya
maendeleo hivyo nao watajitahidi kuhakikisha wanakwenda kufanya kazi
hizo kwa weledi mkubwa hasa ukizingatia taifa linakwenda kasi ili
kukuza uchumi wa nchi.

“Tunaishkuru sana serikali kwa kutuamini wahandisi,ndio maana
tumeandaa warsha hii ili kujadili mambo mazuri ya uendeshaji miradi
nasi tutaishauri serikali nini kifanyike ili tukamilishe miradi kwa
wakati,".

"Pia sisi wahandisi zaidi ya 30,000 tunaahidi kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hasan na kushirikiana nae katika shughuli mbalimbali za ujenzi na kutekeleza miradi ambayo itakuwa na manufaa kwa taifa," amesema Prof Lema

Prof Lema amewataka wahandishi. kujiongeza
kielimu wao wenyewe ili waweze kuendana na wahandisi waliko katika
sehemu nyingine ambazo wanauwezo wa kufanya kila aina ya kazi na kuwahasa kutobweteke katika kazi ya aina moja

Naye Msajili  wa Wahandisi Mhandisi Patrick Barozi alisema mafunzo hayo yataenda sambamba na kutafakali chanzo cha wahandisi wengi wa miradi ya maji kushindwa kutekeleza miradi hiyo kwa wakati na kufanya wahandisi wote nchini kuongelewa vibaya na jamii.

Amesema ukiachana na miradi mikubwa ambayo inatekelezwa hapa nchi ipo miradi ya maji ambayo ilitekelezwa na wahandisi lakini hadi Leo haifanyi kazi katika warsha hii watajua tatizo lilikuwa wapii

" Kwa upande wa miradi ya maji malalamiko yamekuwa mengi hasa yakienda kwa wahandisi, sasa kwenye warsha hii tutajua kwanini malalamiko yanakuwa mengi na tatizo liko wapi na nini kifanyike ilikuondoa malalamiko hayo,"ameeleza


No comments:

Post a Comment

Pages