Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Malongo, akizungumza na wahandisi walioshiriki mafunzo ya usimamizi wa miradi wakati alipokuwa akifungua mafunzo hayo, jijini Dodoma.
NA HAMID RAMADHANI, DODOMA
Kutokana
na hayo serikali imewataka Wahandisi kuhakikisha wanakamilisha miradi
yote mikubwa ya kimkakati iliyoanzishwa na serikali ya awamu tano kwa
lengo la kukuza uchumi na kujenga Tanzania ya viwanda.
Hayo
yalibainishwa leo na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi(ujenzi)
Mhandisi Joseph Malongo wakati akifungua warsha ya siku tatu kwa
wahandisi nakuitaja miradi hiyo kuwa ni Daraja la Salenda,Daraja la
Busisi, Miradi wa kufua umeme na Reli ya kisasa
Amesema
Serikali iliyopitia iliandaa miradi mikubwa ya kimkakati na serikali ya
awamu ya sita imeahidi kutekeleza, waandisi mnajukumu kubwa la
kuhakikisha miradi hii inakamilika kwa wakati kwasababu kukamilika kwake
itakuwa ni chachu ya maendeleo kwa Taifa,
"Katika
nchi hizi ambazo bado zinaendelea sekta ya ujenzi ni muhimu sana
kwasababu inachangia asilimia kubwa ya maendeleo ya viwanda na biashara
hivyo kuongeza ukuaji wa uchumi," alisema
Naye
Mwenyekiti wa Bodi ya Wahandisi Prof Ninatubu Lema amesema wamejipanga
kuhakikisha wanashirikiana na serikali kukamilisha miradi yote mikubwa
ambayo tayari ilishaanzishwa.
Amesema serikali imewapa jukumu hilo la utekelezaji wa miradi hiyo ya
maendeleo hivyo nao watajitahidi kuhakikisha wanakwenda kufanya kazi
hizo kwa weledi mkubwa hasa ukizingatia taifa linakwenda kasi ili
kukuza uchumi wa nchi.
“Tunaishkuru sana serikali kwa kutuamini wahandisi,ndio maana
tumeandaa warsha hii ili kujadili mambo mazuri ya uendeshaji miradi
nasi tutaishauri serikali nini kifanyike ili tukamilishe miradi kwa
wakati,".
"Pia
sisi wahandisi zaidi ya 30,000 tunaahidi kumuunga mkono Rais Samia
Suluhu Hasan na kushirikiana nae katika shughuli mbalimbali za ujenzi na
kutekeleza miradi ambayo itakuwa na manufaa kwa taifa," amesema Prof
Lema
Prof Lema amewataka wahandishi. kujiongeza
kielimu wao wenyewe ili waweze kuendana na wahandisi waliko katika
sehemu nyingine ambazo wanauwezo wa kufanya kila aina ya kazi na kuwahasa kutobweteke katika kazi ya aina moja
Naye
Msajili wa Wahandisi Mhandisi Patrick Barozi alisema mafunzo hayo
yataenda sambamba na kutafakali chanzo cha wahandisi wengi wa miradi ya
maji kushindwa kutekeleza miradi hiyo kwa wakati na kufanya wahandisi
wote nchini kuongelewa vibaya na jamii.
Amesema
ukiachana na miradi mikubwa ambayo inatekelezwa hapa nchi ipo miradi ya
maji ambayo ilitekelezwa na wahandisi lakini hadi Leo haifanyi kazi
katika warsha hii watajua tatizo lilikuwa wapii
"
Kwa upande wa miradi ya maji malalamiko yamekuwa mengi hasa yakienda
kwa wahandisi, sasa kwenye warsha hii tutajua kwanini malalamiko
yanakuwa mengi na tatizo liko wapi na nini kifanyike ilikuondoa
malalamiko hayo,"ameeleza
No comments:
Post a Comment