May 24, 2021

UVCCM YAPAZA SAUTI KUPANDA KWA VIFURUSHI VYA 'INTERNET'

 NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA


MWENYEKITI wa Jumuiya ya  Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM),Kheri James ameiomba serikali kuitafutia ufumbuzi kero ya kupanda kwa gharama za virushi vya Internet (bando), ili kuokoa ajira za vijana wengi waliojiajiri.

Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati alipokuwa akifungua kikao cha Baraza kuu la umoja wa Vijana .

Amesema kuwa, kupanda kwa gharama za vifurushi nchini kuna mchango mkubwa kwa vijana wengi kupoteza ajira zao ambao walikuwa wamejiajiri kupitia mifumo mbambali ya Internet.

“Sio kila anayetumia Internet ni kwa ajili ya kuperuzi tuu meseji mitandaoni wengi hivi sasa wanatumia Internet kwa ajili ya kutangaza biashra zao, kusoma na mtandao hivi sasa ni biashara hili suala lisifumbiwe macho serikali lazima iongeze juhudi katika kutafuta ufumbuzi na kuja na njia itakayo leta nafuu kwa watumiaji”amesema James

Kadhalika amesema kuwa kuna vijana wengi ambao wamejiajiri kupitia mitandao ya kijamii ambao walikosa ajira serikalini, hivyo ipo haja suala hilo kutafutiwa ufumbuzi wa haraka na kuleta nafuu kwa watumiaji.

“Jambo hili serikali tunaona inalifanyia kazi lakini tunaomba juhudi iongezwe kwani vijana wengi wamejiari na wengine kuajiliwa kupitia mitandao ya kijamii, kuna watu wanatangaza bidhaa zao lakini bando ni kikwazo.

“Hatuwezi kuzungumzia Tehama kama hakuna mtandao, hatuwezi kuzungumzia teknolojia kama hakuna matandao wala hatuwezi kuzungumzi mambo ya ubunifu kama bando itakuwa ni kikwazo hivyo tunaomba serikali itafute suluhu ya uhakika kuhusu jambo hili”amesisitiza James

Mwenyekiti huyo pia aliomba serikali kuhakikisha inaondoa urasimu na ukilitimba katika masuala ya uwekezaji kwakuwa hawanga wakubwa katika kero hiyo hua ni kundi la vijana.

“Katika suala la uwekezaji hapa kama serikali itaweka ukilitimba basi wahanga wakuu watakuwa ni vijana na sisi hatupendi hili litoke hivyo basi ni vizuri kila halmashauri kuwa na mikakati yake ya uwekezaji kwa kuwatafuta wawekezeji na siyo kuendelea kusubiri waje”amesema

Pia, aliitaka serikali pamoja na kutoa kipaumbele kwa wawekezaji kuhakikisha kuwa ajira za wazawa zinalindwa kwa gharama yoyote ile.

“Hatutaki kuona katika uwekezaji vijana wetu wanakuwa manamba kwa kupatiwa ajira za ulinzi na ufagiaji tuu bali tunataka kuona vijana wetu wanakuwa na nafasi kubwa katika makampuni hayo”amesema

Vile vile, amesema kuwa Baraza kuu hilo linamapongeza Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuchaguliwa kwa asilimia 100, kuwa mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa.

Amesema UVCCM, itampaushirikiano wa kutosha katika kipindi chote ili kuendelea kuitekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Taifa, Raymond Magwala, amesema kikao hicho kitakuwa na mambo makuu mawili moja ikiwa ni uchaguzi kwa ajili ya kujaza nafasi za wajumbe wa halmashauri kuu ya chama cha Mapinduzi (NEC) bara na visiwani.


No comments:

Post a Comment

Pages