May 23, 2021

KOKA APANIA MAKUBWA KATIKA KUWALETEA WANANCHI CHACHU YA MAENDELEO


Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini wa pili kutoka kushoto akiwa na baadhi ya wabunge wa Mkoani Pwani wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Chama cha mapinduzi (CCM) Taifa waliposimamishwa kwa ajili ya kupatiwa maelekezo kushoto kwake ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikweke.

 Katibu Mkuu wa Chama cha mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo akizingumza na  baadhi wa wanachama na vongozi  wa Mkoa wa Pwani  alipofanya ziara maalumu kwa ajili ya kwenda kujitambulisha akiwa ameambatana na sekretarieti ya chama hicho hawapo pichani(PICHA NA VICTOR MASANGU).

 

 

NA VICTOR MASANGU, KIBAHA 

 

Mbunge wa Jimbo la Kibaha mji Silvestry Koka ameahidi kuyatekeleza maagizo yote ambayo yametolewa na Katibu mkuu wa Chama cha mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo ikiwemo kusimamia suala zima na utekelezaji wa ilani ya chama  kwa kuhakikisha anasikiliza kero mbali mbali za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi wa haraka ikiwemo kulivalia njuga suala la kukithiri kwa mashamba pori lengo ikiwa ni kuleta chachu ya maendeleo kwa wananchi.

Koka aliyasema hayo wakati wa  ziara maalumu  ya Katibu Mkuu wa cahama cha mapinduzi (CCM) Taifa ambaye aliambatana na Sekretarieti ya Chama hicho  kwa ajili ya kuweza kujitambulisha kwa wanachama na viongozi mbali mbali  wakiwemo wakuu wawilaya, wakurugenzi, wenyeviti wa halmashauri pamoja na viongozi wa ngazi ya Mkoa wa Pwani.

 

 

Koka alisema kwamba ujio wa Katibu huyo katika Mkoa wa Pwani umeweza kuleta neema zaidi kutokana na maelekezo ambayo yametolewa ya kuwakumbusha viongozi mbali mbali wa chama kuweza kutekeleza majukumu yao ipasavyo na kuchapa kazi kwa bidii ikiwa ni kutekeleza  miradi mbali mbali ya maendeleo ambayo ipo katika ilani ya chama cha mapinduzi mapinduzi.

 

“Kwa kweli sisi kama wawakilishi wa wananchi tumepokea maelekezo yote ambayo yametolewa na kiongozi wetu amabye ni Katibu mkuu wa Chama cha mapinduzi nagzi ya Taifa, na mimi kama Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini nitahakikisha kwamba maagizo yote amabyo yametolewa ikiwemo suala la kusimamia miradi ya kimikakati nitashirikiana na wenzngu pamoja na serikali ili tuweze kuyasimamia ipasavyo,”alisema Koka.

 

Aidha Mbunge huyo alisema kwamba lengo lake kubwa ni  kuweka mipango madhubuti katika kushirikiana na wananchi kwa kuwasikiliza kero na changamoto zao mbali mbali ili kuweza kuzifanyia kazi na kwamba kuendelea kutekeleza mambo mbali mbali ambayo yameandakwa katika ilani ya chama.

 

Kadhalika alisema kwamba atahakikisha kwamba anasimamia vizuri suala la asilimia kumi ya fedha amabzo zinatolewa na halmashauri kwa ajili ya makundi maalumu ya wakinamama, vijana pamoja na walemavu zinawafikia walengwa kwama ilivyoelekezwa katika maagizo ya serikali pamoja na maelekezo ya Katibu Mkuu wa chama ili makundi hayo yawezae kuzitumia fedha hizo kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi.

 

 

 

 

Kwa upande wake Katibu mkuu wa Chama cha mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo aliwaasa wanachama na viongozi wote kuhakikisha kwamba wanachapa kazi kwa bidii na kuachana na tabia ya kufanya vikao vya kusemana na badala yake wahakikisha wanajadili mambo mbali mbali kwa ajili ya maendeleo kwa wananchi.

 

 

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Chana Cha Mapinduzi (CCM) Bara Christina Mndeme amezitaka Jumuiya za chama hicho kufanyia kazi maadili ya Vijana.

 

Alisema Jumuiya ya Wazazi, Wanawake na Vijana zinatakiwa kufanya kazi hususani maadili ya Vijana kuwaenzi wazee.

 

Naibu Katibu Mkuu huyo alisema viongozi wa chama hicho wanatakiwa kufanya kazi kwa vitendo na si kwenye televisheni na mitandao ya kijamii.

 

 "Kamati za siasa zitenge muda wa kukagua miradi na kutoa ushauri, lakini pia iwepo siku moja ya kusikiliza kero za Wananchi" alisema Mndeme.

 

Aidha alisema kuwa ya wekwe mazingira safi ya uwekezaji urasimu uondolewe ili kuvutia wawekezaji wengi katika Mkoa huo.

 

Alisema wawekezaji wenye maeneo yao wahakikishe wanaanza uwekezaji kwani yatakavyoendelea kuwa mashba pori yatapelekea kuchukukuliwa na Serikali na kupangiwa matumizi mengine.

 

Ziara ya viongozi wa kitaifa wa chama hicho ikiongozwa na Katibu mkuu Da iel Chongolo ilikua na lengo la kujitambulisha na kukumbushana mambo kadhaa ya kufanya wakati wakitekeleza ilani ya Chama Tawala 2020-2025.

 

No comments:

Post a Comment

Pages