Na Lydia Lugakila, Bukoba
Watoto wawili wakazi wa Bukoba mkoa Kagera akiwemo dereva wa gari aina Scania lenye namba za usajili T351BXG wamenusulika kifo baada ya kufunikwa na mzigo wa cement uliokuwa umebebwa na gari hilo mali ya kampuni ya Magu lililokuwa likitokea Dodoma kuja Bukoba kuferi break na kuacha njia kupinduka kisha kuingia kwenye korongo.
Akiwa katika eneo la tukio kaimu Kamanda wa zimamoto mkoa wa Kagera Thomas Majuto amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa 2:50 baada ya gari hilo kuferi break na kupinduka huku dreva wa gari hilo aliyetambulika kwa jina Rwegasira Devid mwenye umri wa miaka 41 kubanwa ndani ya gari hilo, huku watoto wawili waliotambuliwa kwa jina la Avitus Renald miaka (7 )na Switbert Nassoro mwenye umri wa miaka 4 wote wakazi wa Bukoba kunusurika kifo.
Majuto amesema kuwa baada ya juhudi za jeshi la polisi na zimamoto kufika eneo la tukio na kumuokoa dreva huyo pamoja na majeruhi wengine wamefanikiwa kuwapeleka katika hispitali ya rufaa ya Mkoa huo kwa ajili ya matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.
Adha kamanda huyo ameongeza kuwa eneo hilo si sahihi kwa matumizi ya barabara na kuwa sio mara ya kwanza na kuwa kamati husika ya usalama itahakikisha inaweka alama zenye kuonyesha alama za mteremko.
Hata hivyo kwa upande wa wao baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo akiwemo Abdalla Muaga na Bashir wameomba serikali kukarabati maeneo korofi likiwemo eneo la round about ambalo limekuwa likisababisha ajali mara kwa mara.
No comments:
Post a Comment