June 03, 2021

Elimu ya mazingira inahitajika kwa wananchi kuokoa misitu

 

NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA

IMEBINIKA kuwa Tanzania hupoteza zaidi ya Hekta 400,000 za Misitu kwa mwaka kupitia shughuli mbalimbali za binadamu hali ambayo hupelekea mabadiliko ya hali ya hewa ikiwemo ongezeko la joto.

Akizungumza leo jijini hapa ikiwa ni  maadhimisho ya wiki ya mazingira Meneja wa Mawasiliano Shirika la Uhifadhi wa Mazingira Duniani(WWF) Joan Itanisa amesema elimu inahitajika kwa wananchi ilikudhibiti uharibifu wa mazingira.

“Tunafanya kazi na serikali pamoja na wana jamii kuhakikisha tunarejesha uoto wa asili ambao unaharibiwa na shughuli za binadamu ambapo tumeamua kuanzisha kauli mbiu za  uhamasishaji ili kunusuru na kudhibiti hii hali ikiwemo kuanzisha kampeni zinazolinda uoto wa asili,”amesema Joan.

Joani pia ameipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia kwa kuendelea kusimamia Rasilimali za wanyamapoli kwa kuhakikisha zinalindwa kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla.

Amesema kumekuwa na ongezeko la wanyamapoli wakiwemo tembo,vifaru na simba hiyo inadhihirisha kuwa matukio ya ujangili yamepungua kwa asilimia 100.

“Natoa pongezi kwa serikali na wadau wa wanyamapoli wakiwemo WWF kwa kuhakikisha wanapunguza ujangili ambao ilikuwa umeshamili lakini sasa umepungua kwa kiasi kikubwa na kusababisha idadi ya wanyapoli kama tembo na faru kuongezeka na kuongeza idadi ya watalii hivyo kuongeza pato la taifa,”ameeleza

Kwa upande wake Afisa Ulaghabishi wa Sera za Mazingira WWF Nuhu Salala ametaja madhara yatojkanayo na uharibifu wa mazingira kwa binadamu.

Aidha amesema kama hali ya uharibifu wa mazingira itabaki kama ilivyo sasa inaweza kupelekea ongezeko la joto na mabadiliko ya hali ya hewa na mmonyoko wa aridh .

“Kama hatua stahiki zisipochukuliwa za haraka ikiwemo kuanzisha kampeni za kupanda miti ilikurudisha uoto wa asili ulioharibiwa basi tunaweza kushuhudia mabadiliko ya tabia ya nchi ikiwemo jangwa, joto kuongezeka, kubadilika kwa majira, na mafuriko,”ameeleza

Kufuatia maadhimisho ya wiki ya mazingira wananchi wa maeneo tofauti tofauti ya  Mkoa wa Dodoma wamekuwa na maoni mbalimbli na mapendekezo kwa serikali na wadau wa mazingira  kuhusu utunzaji wa mazingira.

Mkazi wa Chamwino Samson Mkoma ameomba serikali kuwawezesha wajasiliamali wa nishati mbadala ili kuwezesha wananchi kupunguza matumizi ya mkaa na kuni katika shughuli za kila siku.

“Wananchi wakiweza kupata elimu kuhusu matumizi ya nishati mbadala kama gesi asilia,mkaa wa chuma itasaidia kupunguza msongamano wa wananchi amabao wanatumia mkaa na kuni ambayo ni hatari kwa mazingira,”amesema

Naye mfanyabiashara wa samaki soko la majengo ameiomba serikali na wadau wa mazingira kuanzisha kampeni sambamba na kutoa elimu ya mazingira kwa wananchi faida za kutunza mazingira,

Amesema wapo wananchi ambao hawana elimu ya mazingira hivyo wanafanya uharibifu bila kujua madhara ambayo yanaweza kujitokeza kupitia uharibifu huo.

No comments:

Post a Comment

Pages