Na Jasmine Shamwepu, Dodoma
MAKAMPUNI ya simu nchini yametakiwa kuboresha huduma kwa wateja pamoja na kushushughulikia changamoto ya matumizi sahihi ya vifurushi na kukomesha tabia ya baadhi ya wafanyakazi wa makampuni hayo kuvujisha siri za wateja wao.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza jijini dodoma, katika kikao chake na wawakilishi wa makampuni hayo, ambacho kilikuwa na lengo la kujadiliana namna bora ya kupeleka mawasiliano katika maeneo ambayo hayana mawasiliano, kilichoandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF).
Akiongea kwenye kikao hicho waziri Ndugulile amesema makampuni hayo yanatakiwa kuboresha huduma kwa wateja kwani kumekuwa na changamoto katika matumizi ya vifurushi kuisha kabla ya muda.
Pia,amesema serikali itahakikisha inapeleka mawasiliano katika maeneo ya mipakani kwa kutoa zabuni kwa makampuni hayo ya simu.
"Nataka kuona makampuni hayo yanafanya maboresho kwa kuhakikisha wanashughulikia changamoto hiyo ikiwa ni pamoja na kulinda siri za wateja pamoja na kuweka mfumo imara wa kusajili namba,amesema na kuongeza;.
Wekeni mfumo mzuri kwa mawakala kwani baadhi wamekuwa sio waaminifu kwani serikali ilitaka kuwafutilia mbali lakini iliona hakuna haja kutokana na kutoa ajira zaidi ya watu 50,000,"alisisitiza.
Waziri ndugulile alisema serikali itaendelea kutoa ruzuku
kwa makampuni hayo ili maeneo ya mipakani mwa nchi yaweze kufikiwa na mawasiliano.
vilevile amesema ni marufuku kwa kampuni yoyote kwa sasa kujenga mkongo bila ya kuomba kibali kutoka wizarani.
Kwa upande wake,mtendaji mkuu wa mfuko wa mawasilino kwa wote (UCSAF), Justina Mashiba amesema lengo la kikao hicho ni kuangalia namna bora ya kupeleka mawasiliano maeneo ambayo hayana mawasiliano kwani lengo la mfuko huo ni kupeleka mawasiliano kwa wote.
“watoa huduma tunahitaji kupeleka mawasiliano nchi nzima na tutatoa zabuni kuhakikisha mawasiliano yanafika mpaka katika maeneo ya vijijini,”amesema.
Naye, Naibu Waziri Wizara ya Mawasilino na Teknolojia yaHabari, Kundo Andrea, alisema kwa sasa mawasiliano ni chakula hivyo kila mtanzania anahitaji kupata mawasiliano hata ambaye yupo kijijini.
No comments:
Post a Comment