Na Jasmine Shamwepu, Dodoma
BARAZA la Taifa la Mashirika yasiyo ya kiserikali (NaCoNGO) linatarajia kufanya uchaguzi wa kitaifa Julai 8, mwaka huu jijini Dodoma.
Baraza litakaloundwa litakuwa na wajumbe 30, kati yao 26, kutoka katika mikoa yote ya Tanzania bara na wajumbe wanne watachaguliwa kutoka katika makundi maalumu ambayo ni pamoja na Mashirika ya kimataifa, watu wenye ulemavu pamoja na watoto na vijana ambapo ifikapo Julai 10, Mwaka huu uchaguzi wa Baraza hilo kuanzia ngazi ya wilaya, mkoa hadi Taifa utakuwa umekamilika na viongozi wapya watakabidhiwa Ofisi rasmi.
Hayo yameelezwa hii leo Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa kamati ya uchagauzi wa NaCoNGO, Wakili Flaviana Charles, alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari wakati akitoa tathimini ya mwenendo wa uchaguzi wa Baraza hilo ngazi ya wilaya uliofanyika Juni26 Mwaka huu.
Aidha, amesema kuwa kwa ujumla uchaguzi ulifanyika kwa amani na utulivu katika wilaya zaidi ya 130, za Tanzania bara ambapo kumekuwepo na mwitikio mkubwa na hamasa ya hali ya juu kwa wagombea na wapiga kura ambapo Uchaguzi katika ngazi ya mikoa yote unafanyika kuanzia leo tarehe 28/06/2021 hadi tarehe 02/07/2021huku Wasajili wasaidizi ngazi wa mikoa watakuwa waangalizi huru wa uchaguzi katika mikoa husika
Hatua hiyo imekuja kufuatia Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Dorothy Gwajima kutoa siku 30, kwa Baraza la Taifa la mashirika yasiyo ya kiserikali (NaCoNGO) kufanya uchaguzi na kuunda Kamati ya mpito ya wajumbe 10 kusimamia uchaguzi huo.
" Hatua hii ilienda sambamba na kutoka ratiba ya uchaguzi ambayo ndani yake ilianisha mambo ya msingi ya kuzingatia kwa mgombea na mpiga kura kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa Baraza la Mashirika yasio ya Kiserikali NaCoNGO ya Mwaka 2016," wamesema Wakili Flaviana.
Wakili Flaviana amesema, zoezi la kuchukua na kurudisha fomu za maombi ya uongozi wa Baraza lilifanyika kuanzia Juni 21 hadi 24 Mwaka huu na uchakataji wa fomu hizo za maombi uliofanyika Juni 25 2021.
Hata hivyo amebainisha kwamba,tathimini ya ujumla katika Wilaya zaidi ya 130 zilizoendesha zoezi hilo nipamoja na kati ya watia nia watano walichukua fomu za kuomba uongozi wa Baraza na jumla ya watia nia wanne walirudisha fomu hizo ambapo zoezi la kuchukua na kurudisha fomu lilifanikiwa kwa takribani asilimia 80.
" Zoezi la kupiga kura lilifanyika Juni 26 Mwaka huu katika Wilaya zote ndani ya mikoa 25 ya Tanzania bara isipokuwa katika Wilaya za mkoa wa kigoma ,ambalo kwa sababu zilizokubalika na pande zote za wasimamizi wa uchaguzi na wagombea na wapiga kura uchaguzi uliofanyika Juni 25 Mwaka huu, huku upande wa Ruvuma kulikuwa na changamoto watafanya uchaguzi wiki hii," amesema Wakili Flaviana.
No comments:
Post a Comment