June 29, 2021

TBS YAADHIMISHA SIKU YA ITHIBATI DUNIANI

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bw. Lazaro Mwambole akifungua maadhimisho ya siku ya Ithibati duniani yaliyofanyika makao makuu ya TBS Ubungo jijini Dar es salaam mapema leo.  

Afisa udhibiti ubora mwandamizi Bi.Stella Mrosso akiongea na wadau wa masuala ya ithibati wakati wa maadhimisho ya siku ya ithibati duniani mapema leo makao makuu ya TBS Ubungo jijini Dar es salaam na kauli mbiu ya mwaka huu ni "ithibati kwa utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu "  

Wadau wa masuala ya ithibati wakifuatilia ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya ithibati Duniani mapema leo Makao Makuu ya TBS Ubungo jijini Dar es salaam na kauli mbiu ya mwaka huu ni "ithibati kwa utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu ".

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

******************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Katika nchi zilizoendelea kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa malengo ya ajenda 2030 ya maendeleo endelevu hufanikiwa kwa kutumia viwango pamoja na huduma zinazotolewa na taasisi zenye ithibati ya Umahiri kwenye upimaji,Ugezi, Ukaguzi na uthibitishaji Ubora.

Katika nchi hizo ithibati ya Umahiri hutumika kama kigezo muhimu kuondoa vikwazo vya kibiashara na kukuza uchumi wa nchi, kukuza pato la taifa na kupunguza umasikini.

Ameyasema hayo leo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw.Lazaro Mwambole katika maadhimisho ya Siku ya Ithibati (Accreditation) Duniani katika Ofisi za Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam..

Aidha Bw.Mwambole amesema Mamlaka zinazotoa ithibati ya umahiri hufanya kazi kwa uhuru bila kuingiliwa wala kuwa na upendeleo.

"Mamlaka hizi zinatekeleza wajibu wao bila kupendelea taasisi zinazozikagua kwa ajili ya kupata cheti cha ithibati au wateja wanaohudumiwa na taasisi hizi". Amesema Bw.Mwambole.

Amesema kuwa ithibati ni moja ya nguzo tatu za miundombinu ya ubora, nyingine zikiwa ni viwango (Standard), Vipimo (Metrology) na udhibiti ubora (Conformity assessment) ambao hujumuisha ukaguzi, upimaji na uthibitishaji ubora.

No comments:

Post a Comment

Pages