HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 07, 2021

TET yadhamiria kupunguza changamoto ya vitabu vya kiada


Na Mwandishi Wetu


TAASISI ya Elimu Tanzania (TET), imekamilisha uandishi wa vitabu aina 29 vya Kiada kwa Shule za Sekondari.

TET chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na jopo lake la wakuza mitaala, wataalam wa elimu kutoka taasisi mbalimbali, walimu kutoka vyuo vikuu vya Tanzania Bara na Zanzibar walianza kazi ya kutoa idhibati aina 29 na watakayoifanya kwa siku tisa.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na TET imeeleza kwamba wataalam hao walikutana na kuanza kazi Juni 02.2021 na kwamba watahitimisha Juni 10.2021.

Taarifa hiyo iliainisha vitabu hivyo vya kiada kwa sekondari kuwa ni Biology Kidato cha Kwanza, Biology kidato cha Pili, Biology Kidato cha Tatu.

Vingine ni Home Economics Kidato cha Kwanza, Home Economics Kidato cha Pili, Kiswahili Kidato cha Kwanza, Kiswahi Kidato cha Pili, Kiswahili Kidato cha Tatu, Civics Kidato cha Kwanza na Civics Kidato cha Pili,

Vitabu vingine ni Physics Kidato cha Kwanza, Physics Kidato cha Pili, Chemistry Kidato cha Kwanza, Chemistry Kidato cha Pili, ICS Kidato cha Kwanza, ICS Kidato cha Pili na ICS Kidato cha Tatu.

“Basic Mathematic Kidato cha Kwanza, Basic Mathematics Kidato cha Pili, Basic Mathematics Kidato cha Tatu, Basic Mathematics Kidato cha Nne, Geography Kidato cha Tatu, Geography Kidato cha Nne, History Kidato cha Tatu.

“...English Kidato cha Tatu, English Kidato cha Nne, English Listening activities Kidato cha Tatu na Nne, Agriculture Kidato cha Kwanza na Angriculture Kidato cha Pili.

“Vitabu hivi sasa vipo katika hatua ya kupitiwa na kupewa ithibati na Kamishna wa Elimu pamoja na jopo lake,” ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo.

Kukamilika kwa kazi hiyo kutapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto ya upatikanaji wa vitabu vya Kiada kwa Shule za Sekondari hapa nchini na kuwa msaada kwa wanafunzi.

No comments:

Post a Comment

Pages