June 29, 2021

Wadau watakiwa kuwasaidia kiuchumi waathirika wa dawa za kulevya



 

Na Jasmine Shamwepu, Dodoma


WAZIRI M
kuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema kuwa tatizo la matumizi ya Dawa za kulevya Nchini limeendelea kuongezeka siku hadi siku huku akitoa Maelekezo mbalimbali  kwa wadau  katika kuwasiadia  waathirika wa dawa za kulevya kiuchumi ili wasirudi katika matumizi ya Dawa hizo.
 

Maelekezo hayo yametolewa hii leo Jijini Dodoma na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene kwaniaba ya Waziri Mkuu katika Maadhimisho ya Kilele Cha siku ya mapambano ya Dawa za kulevya ambayo Kitaifa yamefanyika Mkoani Dodoma.


Sanjari na hilo  ametaka kuangaliwa kwa mitaaala  ya Elimu kwa kuongeza somo la dawa za kulevya ili kuweza kuliokoa kundi la Vijana ambalo lipo hatarini katika matumizi ya Dawa za kulevya.
 

Awali akitoa taarifa kuhusiana na mapambano ya Dawa za kulevya, Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kuzuia na  kupambana na Dawa za kulevya Nchini, Gerald Kusaya ameeleza jitihada zinazofanywa na Mamlaka hiyo huku akieleza changamoto zinzazowakabili.

 
Kwa upande wao Wadau wa maendeleo akiwemo Balozi wa Italia Nchini Tanzania, Marko Lombadi, John Mark ambaye ni mpelelezi kitengo cha  kupambana na Dawa za kulevya wa Umoja wa Nchi za ulaya UK wakeleza athari za madawa ya kulevya na kuahidi kushirikiana na Serikali katika mapambano ya Dawa za kulevya ili kuweza kutokomeza matumizi ya Dawa hizo ambazo zimekuwa na athari kwa jamii na Taifa kwa ujumla.

 
Nao baadhi ya Waraibu wa Dawa za kulevya walikuwa na haya ya kusema.


Maadhimisho hayo yalianza rasmi Juni 23 ambapo Kilele chale kimehitimishwa Juni26 yakibebwa na kauli mbiu isemayo "Tuelimishane kuhusu tatizo la Dawa za kulevya kuokoa Maisha.

No comments:

Post a Comment

Pages