June 29, 2021

Zaidi ya kampuni 3000 kushiriki Maonyesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF)

 


Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo.

 

 

Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam

NCHI saba  za kigeni  na kampuni 76 kutoka katika nchi hizo  zinashiriki  kwenye Maonyesho ya  45  Biashara ya Kimataifa  ya Dar es Salaam (DITF), ambayo yameanza jana na kufunguliwa rasmi Julai 5 mwaka huu.

Pia Wizara ya Viwanda na Biashara kupitia taasisi yake ya Mamlaka ya Maendeleo  ya Biashara  ( Tan Trade), tayari imeshakamilisha  maandalizi ya Maonyeshoya hayo.

Akizungumzia jijini Dar es Salaam jana Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo  amesema hadi saaa jumla ya washiriki zaidi ya 3000 wanashiriki  na kwamba washiriki hao ni  pamoja na makampuni ya ndani.

"Nitoe wito kwa kampuni, taasisi za Umma na buashara kujitokeza kwa wingi kutunia fursa hii muhimu kujitangaza kibiashara," anesema.

Waziri huyo  ameongeza kuwa Tan Trade inaendelea kushirikiana na sekta ya Umma na binafisi ili kufanikisha  maandalizi ya Maonyeshoya hayo.

Amewashukuru wadau mbalimbali kwa kusndelea kushiriki Maonyesho hayo  na baadhobyq kamupuni zilizodhamini  ni pamoja na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Shirika la Bima la Taifa(NIC), Benki ya CRDB. King Lion Investment, Africa Media Group , Mikoani  Traders (Azania Group of Companies,MIC ,Tigo, Vodacom.

Ameongeza kuwa mwaka huu wa 2021 moonesho hayo yanatimiza Mika 45 tangu yalipoanzishwa na kwamba kutakuwa na mitaa maalumu kama vile mtaa wa kilimo , madini Viwanda vidogo wajasiriamali wadogo na wasanii

No comments:

Post a Comment

Pages