July 02, 2021

Benki ya PBZ yajivunia kuwepo kwa serikali ya Muungano


 

 

Afisa  Mwandamizi Masuala ya Masoko na Uendeshaji wa Biashara kutoka Benki ya PBZ. Mohamed Khamis Ismail  akitoa maelezo  kwa wateja waliotembelea banda la benki hiyo  katika  Maonyesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) maalufu Sabasaba.


Na Asha Mwakyonde Dar es Salaam

AFISA Mwandamizi Masuala ya Masoko na Uendeshaji wa Biashara kutoka Benki ya PBZ. Mohamed Khamis Ismail  amesema kuwa kuwapo kwa serikali ya  Muungano, benki hiyo imeweza kujitanua kutoa huduma za za kifedha Tanzania Bara na Zanzibar.

Pia vikundi mbalimbali vimeshauriwa kuchangamkia fursa katika kipindi hiki cha maonyesho ya sabasaba kutembelea banda lao ili kupata elimu ya huduma mbalimbali za kifedha kwa ajili ya kuendeleza miradi yao.

Pia benki hiyo ya PBZ imesambaza  huduma za kibenki zinazotolewa na benki hiyo katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar na Tanzania Bara huku ikichangia kwa kiwango kikubwa kutangaza umuhimu wa Muungano.

Akizungumza katika Maonyesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) maalufu Sabasaba yenye kauli mbiu ' Uchumu kwa Ajira na Biashara Endelevu'.

Ismail amesema zipo faida nyingi ambazo zimeletwa na uwapo wa Muungano huo  PBZ  imekuwa ikitoa huduma za kifedha hasa kwa vikundi vya wakulima katika mikoa mbalimbali katika pande zote za muungano .

Ismail amesema kilimo na kinahitaji maandalizi ili kukamilika ikiwq ni pamoja na kuandaa mashamba hivyo benki ya PBZ inatoa mikopo kwa vikundi vya wakulima lengo likiwa ni kuwainua wakulima kiuchumi.
 
"Tuna farijika  uwepo wa muungano una faida kubwa na PBZ tumetumia huduma zetu kuendelea kuutangaza hasa katika kuhakikisha wananchi wote wananufaika kupitia taasisi hii ya fedha kuinua uchumi, amesema Ismail.

Amesema wanufaika wa benki hiyo ni wanachama ambapo wapo katika vyama vya ushirika wa  wakulima (AMCOS), kwani chama hicho kinawasimamia wakulima vizuri. kwani vinwtambulika kisheria.

"Tumekuwa tukitoa mkopo kwa makundi ya wakulima wa korosho na karafuu na ni nafuu kwa sababu lengo lake ni kutaka viboreshe kilimo chao zaidi, kukuza uchumi wao na wa nchi kwa ujumla,"amema Ismail.

Ameongeza kuwa ili kupanua wigo wa utoaji wa huduma zao zaidi,  wamejipanga kujitanua katika mikoa yote ya pande zote za muungano. 

 

Amesema kwa sasa wanatoa huduma Zanzibar na katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, na Mbeya.

"Maonyesho ya Sabasaba ni fursa kubwa sana, wanatakiwa kuichangamkia, wakija hapa PBZ watafahamu aina ya mikopo wanayotakiwa kuchukua na niwashauri waondoe ile dhana ya kuogopa kuchukua mikopo kwenye taasisi za kibenki bila kufika na kupata elimu sahihi, wasisikie yale wanayoambiwa, wakumbuke kwamba uchumi wao na wa nchi utakuwa bora kwa kufanya kazi kwa bidii kama Rais Samia Hassan Suluhu anavyotusisitiza kila mara, amesema Ismail.

No comments:

Post a Comment

Pages