July 06, 2021

Benki ya Stanbic yazindua Kampeni ya Madawati Initiative kutoa madawati 2000 kuboresha sekta ya elimu


 
Hussein Ndubikile, Dar  es Salaam

Benki ya Stanbic imezindua Kampeni ya Madawati Iniative huku ikibainisha kupitia kampen hiyo itatoa madawayti 2000 kuboresha miundo mbinu ya Sekta ya elimu nchini.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Mkuu wa Idara ya Wateja wa Rejareja wa benki Omari Mtiga amesema wameamua kutoa madawati hayo kwa kuwa takwimu zinaonyesha bado kuna upungufu mkubwa na kwamba watatoa kila mwaka kuiunga mkono Serikali.

Amebainisha kuwa benki hiyo ina miaka zaidi ya 20 na tangu ianzishwe imeshachangia zaidi ya Sh Bilioni moja kuchangia sekta ya afya na elimu huku akiwaomba wadau wengine kuchangia kuboresha sekta hiyo.

" Leo tunazindua kampeni hii mahsusi ya kuunga juhudi za Serikali kuboresha miundo mbinu ya elimu kwa kuanzia tutatoa madawati 2000 hatutaisha hapa kila mwaka tutachangia," amesema Mtiga.

Amesisitiza kuwa benki hiyo ina utaratibu wa asilimia moja kila mwaka kuchangia jamii hivyo katika miaka mitano iliyopita iltoa Sh bilioni moja kuboresha sekta ya elimu na afya.

Kwa upande Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Ndalichako ameishukuru benki hiyo kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali kuboresha miundo mbinu ya elimu hivyo inaonyesha jinsi gani wanavyoijali jamii.

Profesa Ndalichako amesema bado Serikali inaendelea kuboresha miundo ya sekta hiyo kwa kuongeza matundu ya vyoo, ujenzi wa majengo na mabweni ya watoto wa kike na kusisitiza utaratibu wa elimu bure uanachangia changamoto kutokana na kuongezeka kwa wanafunzi.

Naye Mkuu wa Idara wa Masoko wa benki hiyo Desidera Mwegelo amesema wameamua kuiunga mkono Serikali kwa namna moja au nyingine kutokana na uhitaji wa madawati katika shule nchini na kwamba kampeni hiyo imebeba kauli mbiu isemayo Pamoja Elimu Bora Inawezekana.



No comments:

Post a Comment

Pages