July 06, 2021

Edna Sunga azindua EDNA SUNGA CONNECTION kuisaidia jamii

Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


Mwanasiasa, Edna Sunga amezindua kipindi cha Tv cha Edna Sunga Connection chenye lengo la kuisaidia jamii yenye matatizo mbalimbali pamoja na kuwasaidia watu wenye vipaji ambao hawajapata nafasi ya kusikika wala kuonekana.

Akizindua kipindi hicho leo jijini Dar es Salaam Edna amesema ameamua kuanzisha kipindi hicho kutokana na kupitia changamoto mbalimbali za kimaisha na kwamba jamii itapata fursa ya kuonyesha viapaji ilivyonavyo na kusaidiwa kutatua matataizo yanayoikabili.

Amebainisha kuwa kipindi hicho kwa sasa kimeanza kuonyeshwa katika EDNA SUNGA TV  kupitia cheneli ya Youtube na kwamba kitasaidia kuona vipaji vingi na vikubwa visiotumika au kunyimwa nafasi.

" Watu wengi wananifahamu kama mwanasiasa hawajui nilianzia niliingia katika siasa nikitokea kanisani  kwa lengo moja tu  Mungu anitumie kulisaidia taifa langu na watu wake kwa vile wanavyotakiwa kuwa na haki," amesema Edna.

Amesisitiza kuwa kuna vipaji vingi katika jamii ambavyo havijapewa nafasi wakiwemo wasanii wa maigizo, wanamitindo, Mamc, waimbaji wa nyimbo za dini pamoja na wanamuziki hivyo kupitia kipindi hicho watapata fursa ya kujulikana kwa kuunganishwa katika sehemu husika.

Ameongeza kuwa kipindi hicho kitatoa usaidizi kwa wanawake waliokataliwa watoto wao na waume zao na kukosa haki ya malezi ya watoto hivyo kitatoa msaada jinsi ya kupigania haki zao.

Katika hatua nyingine kabla ya uzinduzi huo Edna aliwashukuru wanasiasa kwa mchango wao uliomjenga akiwezi Zitto Kabwe, Humprey Polepole na wengine waliomjenga kisiasa.

Kwa upande wa Meneja wa Hotel ya Centre Point ambao ndio wadhamini wa kwanza wa kipindi hicho Edwin Sigge amesema wameamua kumuunga mkono Edna kwani anaonyesha kujituma na kuwa dhamira ya dhati kuisaidia.

Naye Mtoto wake Edna, Lisa Brown amesema yupo pamoja na mama yake kuisaidia jamii yenye matatizo na kwamba anamuunga mkono Rais Samia Suluhu.



No comments:

Post a Comment

Pages