July 08, 2021

GCLA kufanya uchunguzi wa watoto wanaozaliwa na jinsia mbili

Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), imesema kuwa Mamlaka hiyo kwa kushirikiana na madaktari mbalimbali nchini inafanya uchunguzi kwa watoto wanaozaliwa na jinsai mbili tofauti .

Akizungumza katika Maonyesho ya 45 ya Biashara ya Kimatafa DITF yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Huduma na Udhibiti anayesimamia Uingizaji, Usambazaji na Matumizi ya Kemikali nchini kutoka mamlaka hiyo, Daniel Ndiyo
aliseema lengo kuangalia kuangalia ipi inanguvu na inaweza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Ndiyo alisema watoto wanaozaliwa na jinsi mbili tofauti wapo ingawa wanafichwa hivyo mamlaka inaiomba jamii kuacha kuwaficha na kuwaleta kwenye mamlaka hiyo ili waweze kupimwa na kufanyiwa uchunguzi.

"Kwa sasa hakuna haja ya kuwaficha watoto hao, Mkemia Mkuu wa Serikali anatoa huduma ambapo kwa kushirikiana na madaktari mbalimbali wanafanya uchunguzi wa kudhibitisha ni jinsi gani ambayo inatawala kati ya kiume na kike," alisema

Alisema wanapofanya uchunguzi wa kimaabara wanaweza kutambua kwamba mtoto huyo ni mwanamke au ni mwanaume hivyo jinsi ambayo haitakiwi kuwepo wanawashauri madaktari kuweza kufanya upasuaji ili kumuweza mtoto huyo atambulike kama ni mwa kiume au wa kike.


Pia alisema mamlaka hiyo
inafanya uchunguzi wa vinasaba kwa wagonjwa wa figo, kama mtu ana ndugu mwenye matatizo ya figo na anahitaji kutoa figo kwa mgonjwa ni lazima atapimwa ili kuangalia kama zinahusiana au kuwiana.

"Sisi sasa ndio tunafanya uchunguzi  kudhibitisha kwamba watu hao wawili mgonjwa na mtoaji wa figo, figo zao zinawiana, tukigundua zinawiana tunawashauri madaktari wanaendelea na upasuaji wa upandikizaji wa figo," alisema

Aliongeza kuwa katika masuala hayo ya uchunguzi wa figo wamekuwa wakishirikiana na hospital mbalimbali nchini ikiwemo Hospital ya Taifa ya Muhimbili  (MNH) na Aga Khan.

Hata hivyo alisema mamlaka hiyo inatekeleza sheria ya masuala ya usimamizi na udhibiti wa kemikali mbalimbali zinazotengenezwa na kuingizwa nchini.

Aidha alisema lengo kubwa la kushiriki maonesho ya mwaka huu ni kuikumbusha jamii majukumu ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali GCLA na shughuli wanazozifanya.

"Kwa ujumla majukumu yetu ni mengi ambayo tutawaeleza wananchi lakini tunayomajukumu manne tunayoyafanya ambapo la kwanza ni uchunguzi wa kimaabara wa sampuli mbalimbali ambazo zinafanyika katika maeneo mawili moja ni za jinai na kijamii," alisema

Alisema sampuli za jinai ni pamoja na masuala yanayohusiana na ubakaji, wizi, dawa za kulevya, sumu na sampuli za kijamii ni kuthibitisha ubora wa maji mara baada ya kuchimba kisima cha maji

No comments:

Post a Comment

Pages