Na Jasmine Shamwepu, Dodoma
BARAZA la Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali (NaCoNGO) limepata viongozi wapya ambapo Mwenyekiti mpya wa Baraza hilo, ni Lilian Badi.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo,leo Julai 8,2021,Mwenyekiti wa Kamati ya mpito iliyosimamia uchaguzi huo,Flaviana Charles amemtaja Badi kuibuka na ushindi mara baada ya kupata kura 21 huku Jane Magigita akiambulia kura 8.
Katika nafasi ya Katibu Mkuu,wajumbe hao wamemchagua Revocatus Sono kwa kura 22 huku Gifti Kilasi akiambulia kura 7.
Nafasi ya Mwekahazina wajumbe hao wamemchagua John Kiteve kwa kura 15 huku Miraji Malinda akipata kura 13 na nafasi ya Kamati ya Fedha na Utawala wamempigia kura za ndio Gaidon Haule ambaye alikuwa peke yake katika nafasi hiyo.
Katika kamati ya maadili wajumbe hao wamemchagua Novatus Marandu ambaye amepata kura 15 na Kamati ya Maendeleo na Uwezo akichaguliwa Rhobi Samweli, Kamati ya Utandaa na Mawasiliano akichaguliwa Asifiwe Mallya huku wajumbe wanne wa Bodi wakiwa ni Jane Magigita,Revocatus Sono,Paulina Majogoro na Baltazari Komba.
Mjumbe wa kamati ya mpito iliyoteuliwa na Waziri wa Afya kuhusu uchaguzi, Yasin Ally amesema uwepo wa baraza hilo itasaidia kuratibu kikamilifu mchango wa mashirika yasiyo ya kiserikali .
Akizungumza mara baada ya kutangazwa kwa matokeo Mwenyekiti mpya Baraza hilo, Lilian Badi ameomba ushirikiano huku akiahidi kutekeleza yale ambayo aliahidi wakati wa kuomba kura.
Kwa upande wake,Katibu mpya wa Baraza hilo, Revocatus Sono amewashukuru wote waliomwamini kwa kumpigia kura ambapo amedai kwamba mchakato huo haukuwa mdogo.
Ikumbukwe kuwa kufanyika kwa uchaguzi huo imetokana na agizo la Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee, Dkt. Dorothy Gwajima alilolitoa hivi karibuni kwa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali (NaCoNGO) kufanya uchaguzi kama ilivyo kwa mujibu wa sheria ya baraza la mashirika yasiyo ya kiserikali ambapo inaelekeza kufanyika uchaguzi kila baada ya miaka mitatu ambapo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Uzinduzi wa baraza jipya la NaCoNGO jijini Dodoma.
July 08, 2021
Home
Unlabelled
Matokeo ya Viongozi wapya NaCoNGO Yatangazwa.....
Matokeo ya Viongozi wapya NaCoNGO Yatangazwa.....
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment