HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 07, 2021

Ndalichako ataka wahitimu vyuo watatue changamoto ya ajira

 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika ofisi za Tantrade zilizopo katika viwanja vya maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, akizungumza jambo na Naibu waziri wa wizara hiyo, Omary Kipanga.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, akitembelea maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

 

Na Selemani Msuya

 

TAASISI za elimu ya juu nchi zimetakiwa kutoa elimu ambayo itatoa wahitimu wenye ujuzi wa kujiajiri ili waweze kutatua changamoto ya ajira kwenye jamii.

Aidha, taasisi wabunifu wametakiwa kubiasharisha bunifu zao ili ziweke kuingia katika soko la ushindani na kutumia na jamii.

Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Maonyesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) maarufu Sabasaba yenye kauli mbiu ' Uchumu kwa Ajira na Biashara Endelevu'  yanayofanyika katika Viwanja vya Julius Nyerere Temeke jijini Dar es Salaam.

Waziri Ndalichako ambaye aliambatana na Naibu Waziri Omary Kipanga, alisema katika matembezi hayo amejifunza mambo mengi ambayo yanafanywa na taasisi zake ambayo yanaweza kusaidia kubadilisha maisha ya jamii ya Kitanzania.

Alisema Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza kuwa elimu ya Tanzania itoe watu wenye ujuzi hivyo ni vema taasisi za elimu zote zijikite katika eneo hilo ambalo litaweza kutatua changamoto ya ajira.

Prof. Ndalichako alisema taasisi zote ambazo zipo chini yua wizara yake zina jukumu la kutoa elimu, utafiti na kutoa huduma za jamii na kwa asilimia kubwa wamefanya vizuri hivyo anasisitiza nguvu iongezwe zaidi.

Alisema kwa sababu taasisi zimefanikiwa katika maeneo hayo matatu hivyo ni wakati muafaka utatuzi wa changamoto katika jamii unaonekana moja kwa moja kupitia vijana ambao wanahitimu vyuo husika.

“Wapo vijana ambao wamepatiwa elimu, wakafanya utafiti na kubuni mambo mbalimbali hivyo ni vyema bunifu zao zikaendelezwa ili ziweze kusaidia kutatua changamoto ya jamii.

Ujuzi ambao wanaupata hautakuwa na tija kama vijana wanakaaa mitaani baada ya kumaliza shule hivyo ni vema taasisi kama Tume ya Sayansi na Teknolojia  (COSTECH) kupitia mashindano yake ya Makisatu kuendeleza vijana ambao wanakuwa wabunifu kwa kubiasharisha kazi zao,” alisema.

Alisema wizara yake itashirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara kuhakikisha bunifu ambazo zinafanywa na vijana wa Kitanzania zinabiasharishwa ili ziweze kujibu c hangamoto ya ajira.

Waziri Ndalichako alisema pamoja na kuwezesha wabunifu pia taasisi hizo ziendelee kutoa ushauri na kusaidia kuandika maandiko ambayo yataweza kushawishi wadau kusaidia katika eneo hilo.

“Sisi kama wizara tutahakikisha kazi za wabunifu ambazo zinatmbulika COSTECH zinabiasharishwa ili zitumike kusaidia kuongeza ajira nah ii ndio kauli mbiu ya mwaka huu,” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa COSTECH alisema wamekuwa wakipokea changamoto mbalimbali baada ya kuwezesha wabunifu na watafiki hivyo wamejipanga kuendelea kushirikiana ili kuweza kuzitatua.

Alisema katika hilo wanatarajia leo kukutana na Waziri pamoja na wanufaika mbalimbali wa COSTECH kujadaili namna ya kufikia mwisho wa kile ambacho wanakibuni au kutafiti ili kisiishie katikati.

“Kesho (Leo) tutakutana na wfanyabiasharam sekta binafsi, watafiti, wabunifu na wizara ambapo tutajadili ni wapi tunakwama hata kama tumewezeshwa katika utafiti na ubunifu wetu. Imani yangu tutatoka salama hasa katika hii changamoto ya masoko,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Pages