July 01, 2021

SBL yazindua Kampeni ya Tunyanyuke Pamoja, kutoa Sh Bilioni 2.3 kukabiliana na Corona



Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Kampuni ya Bia ya Serengenti (SBL) imezindua Kampeni ya Tunyayuke Pamoja na kubainisha kuwa kupitia kampeni hiyo itatoa Sh Bilioni 2.3 kwa ajili ya kukabiliana na Ugonjwa wa Corona (Covvid-19).

Akizugumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo leo jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Mark Occiti amesema kampeni itawalenga wamiliki wa baa,wateja na wafanyakazi wa baa na kwamba fedha hizo zitatumika katika tahadhari ya ugonjwa huo kwa kuweka sehemu za kunawia mikono, vitakasa mikono, viti na maturubai kwa baa zote zitakazopata nafasi.

Amebainisha kuwa kampeni hiyo itazilenga baa 2000 katika mikoa mitatu ikiwemo Dar es Salaam, Arusha na Zanzibar na kwamba kuna vigezo vitatumika  ili baa ipate fursa ya kuingia kwenye kampeni hiyo.

Amesisitiza kuwa kampeni hiyo itasaidia wamiki hao na wafanyakazi na wateja wao kujihadhari na ugonjwa huo  kwani watatakiwa kuzingatia kanuni za usafi zitakazowekwa katika maeneo ya baa.

Mkurugenzi huyo amesema SBL imezindua kampeni ikiwa ni mwendelezo wa kampuni hiyo kukabiliana na ugonjwa huo na kwamba mwaka jana walitoa vitakasa mikono, vipeperushi vya kutoa elimu ya Corona kwa umma.

Aidha amesema kampeni hiyo itasaidia kuwainua kimauzo wateja wao kwani mwaka jana hali ya biashara ilikuwa mbaya kutokana na ugonjwa huo hivyo wanaamini wamiliki watachangamkia fursa hiyo kwa kujisajili.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni hiyo John Wayancha amesema wamiliki wa baa watatakiwa kujisajili katika mtandao wa SBL ili wapate baada kukidhi vigezo vilivyowekwa ikiwemo ukubwa wa baa na uwepo baa mwaka mmoja kabla ya Corona.

Amesema kuwa mpango kampeni hiyo ni ya miaka 2 na kwamba imelenga mikoa hiyo kutokana na kuwa hatari ya maambukizi ya Corona sababu ya mwingiliano wa watu hasahasa wageni wanaoingia mikoani humo.

Naye Msambazaji wa Bia za SBL, Kevin Tegwa ameipongeza na kuishukuru kampuni hiyo kwani inaonyesha jinsi inavyowajali wateja wake katika kuwasaidia kujihadhari na ugonjwa huku wakiendelea na shughuli zao.

Mfanyabiashara Mramba amesema mwaka jana mauzo yalidorora kutoka na watu kuhofia ugonjwa na kwamba kupitia kampeni hiyo anaamini watafanya biashara katika mazingira salama. 


No comments:

Post a Comment

Pages