July 01, 2021

POLISI DSM YASEMA HAITAWAVUMILIA VIJANA WAHALIFU

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewatahadharisha vijana ambao ni wahalifu waishio kwenye viunga vya Mkoa huo kuachana na matendo hayo na kwamba Jeshi hilo litahakikisha wanawakamata na kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobaika kutenda makosa hayo.


Hayo yameelezwa na kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ACP Muliro  Jumanne wakati akiongea na Waandishi wa habari kwenye Ukumbi uliopo Makao Makuu ya Polisi  Dar es Salaam.


Kamanda Muliro amesema vitendo vya uporaji imekua ni kero kubwa Jijini Dar es Salaam na kutoa onyo Kali Kwa vijana wote wanaofanya vitendo hivyo.


Kamanda Murilo alisema kwenye operesheni ya kupambana na vitendo vya uporaji na uvunjaji wa nyumba wameweza kukamata mali za  Simu,TV,Laptop n.k zilizoibiwa katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huo


Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam imekamata Silaha mbili aina ya Bastola na hii ni kutokana na ushirikiano mzuri baina ya wananchi na Jeshi Hilo 


Sambamba na hilo alitumia wasaaa huo kuwapongeza Wannachi kwa mashirikiano makubwa wanayoyatoa ili kuhakikisha vitendo vya uhalifu vinadhibitiwa na kuondoka katika Mkoa huo


Alisisitiza kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na operesheni mbalimbali katika kuhakikisha wanadhibiti matukio ya uhalifu na uvunjaji wa sheria za Nchi

No comments:

Post a Comment

Pages