July 01, 2021

TANTRADE YAWATAKA WAZALISHAJI BIDHAA KUZINGATIA MASHARTI YA UUZAJI


 Kaimu Meneja wa Uendelezaji Bidhaa kutoka  Mamlaka  ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Masha Hussein, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.

 

Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam

MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), imesema bado  kuna tatizo la kukosa elimu ya kuhusiana na uzalishaji na namna ya kuweka vifungashio vyenye taarifa zinazojitosheleza hasa zinapokwenda kuuzwa nje ya nchi.

Pia Mamlaka hiyo imetoa ushauri kwa wazalishaji wa bidhaa nchini kuzingatia masharti ya uuzaji na uzalishaji wa bidhaa zinazouzwa katika soko la kimataifa ili kuteka soko hilo kwa ukubwa.

Akizungumza katika mkutano wa ana kwa wadau wa uzalishaji na uuzaji wa bidhaa za nyama, matunda ya Parachichi kwa njia ya mtandao ukihusisha wadau kutoka nchi za Saudi Arabia, Kuwait,Qatar na Nchi za Falme za Kiarabu, Kaimu Meneja wa Uendelezaji Bidhaa kutoka TANTRADE, Masha Hussein amesema mkutano huo ulilenga kujadili hatua za uuzaji wa bidhaa hizo katika nchi husika.

"Na ndio maana tumepanga kwamba tuanze kutoa elimu za mara kwa mara kwa wafanyabiashara hawa ili wajue mbinu mbalimbali kupambana na kuchangamkia fursa hizi, "amesema Hussein.


Amesema pamoja na Tanzania kuwa na idadi kubwa ya mifugo, lakini bado kiwango cha nyama kinachouzwa katika nchi zenye uhitaji ni kidogo kuliko malengo.


"Kwa mfano Tanzania sisi tuna mifugo mingi sana lakini ukiulizwa ni kiwango kinachouzwa kwenye hizo nchi zinazohitaji ni kidogo sana na haijafikia kile kinachohitajika katika nchi hilo, "amesema Hussein.


Aidha amesema mwitikio wao wa kijitokeza kuchangakia fursa hizo ni mkubwa  lakini shida huwa inakuja kwenye kutekeleza masharti yake yanayokuwa yamewekwa kwa wauzaji wa bidhaa hizo katika kila nchi husika.

No comments:

Post a Comment

Pages