July 09, 2021

TOAM, AMMI kukutanisha wadau 300 wa Kilimohai

Mwenyekiti wa TOAM, Dk. Mwatima Juma akizungumzia maandalizi ya kongamano la Kilimohai litakalofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya wanahabari waliohudhuria mkutano wa Mwenyekiti wa TOAM, Mwatima Juma kuhusu maandalizi ya Kongamano la Kilimohai litakalofanyika jijini Dodoma, Oktoba mwaka huu.

Na Mwandishi Wetu

MTANDAO wa Kilimohai Tanzania (TOAM) na Kampuni ya AMMI wanatarajia kukutanisha wakulima na wadau wa kilimohai zaidi ya 300 kutoka nje na ndani ya nchi kwenye Kongamano la pili litakalofanyika jijini Dodoma.

Kongamano hilo la siku mbili litengeneza mkakati maalum wa kukiendeleza kilimohai na kupata mrejesho wa maazimio ya kongamano la mwaka 2019 na kuongeza uelewa wa kilimohai kwa watanzania wengi zaidi.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo Julai 09.2021 Mwenyekiti wa TOAM, Mwatima Juma anasema kongamano hilo litasaidia kufikiwa kwa malengo ya mtandao huo ya kumrejesha mwanadamu kwenye uasili wake huku akifafanua kwamba kilimohai ni kile kisichotumia kemikali.

“Suala la kilimohai linatakiwa kuwa la kitaifa ifike pahali serikali ione ulazima wa kilimohai na kukitengenea idara sio dawati, kilimohai kitengewe bajeti yake wananchi wakielewe.

“...Mathalani suala la mbegu ni biashara ya matajiri, sisi tunataka kwanza serikali itusaidie kwenye tafiti za mbegu za asili ambazo mazao yake yataonesha tija kwa mkulima,” anasema Mwatima.

Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, kongamano hilo litatoa fursa kwa wadau wa kilimohai kukutana, kubadilishana mawazo na kujua mbinu wanazotumia wengine kwenye shughuli za kilimohai.

Anasema kongamano hilo litatoa mwelekeo wa kufikia hatua nzuri ya kuwa na uhakika wa usalama wa chakula, afya ya mlaji, udongo na mazingira kupitia kilimohai.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao kutoka Wizara ya Kilimo, Beatus Malema alisema serikali inalo dawati la kushughulikia kilimohai na kusema juhudi zinaendelea kufanyika ili kuikuza sekta hiyo.

Mratibu wa kongamano hilo kutoka AMMI, Vida Makamba amewaalika wadau wengine kushiriki kwenye maandalizi ya shughuli hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages