July 09, 2021

Wafanyabiashara washauriwa kutumia mfumo wa e-shop

 

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan trade), Balozi Mteule Edwin Rutageruka (kushoto) na Kaimu Posta Masta Mkuu, Macrice Mbodo, wakifurahira mara baada ya uzinduzi wa mfumo wa Duka Mtando (e-shop).

 


Asha Mwakyonde, Dar es Salaam

WAZIRI  wa Habari,  Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia  Dkt. Fautine Ndugulile amewataka wafanyabiashara, wajasiriamali na wenye viwanda kutumia mtumo wa duka mtandao (e-shop), ili kuuza na kununua bidhaa zao popote walipo

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania na Shirika la Posta Tanzania wa Uendeshaji wa Duka Mtandao

Hayo aliyasema wakati akizindua mfumo huo katika  maonyesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF), yanayoendele kufanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere yenye kaulimbiu ya  ' Uchumi wa Viwanda Ajira kwa Vijana  na Biashara Endelevu" wakati wa Uzinduzi wa Ushirikiano wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania na Shirika la Posta Tanzanian wa Duka Mtandao (e_shop).

'Dkt. Ngugulile amesema katika mtandao huo mfanyabiashara atapata fursa ya kununua na biashara  zao.

Amesema Kazi yao  ni kuunganisha masula ya habari na ekenolojia na kwamba Wizara hiyo imeanzishwa mahusu kuhakikisha masula ya mbalimbali ya kijamii yanaendelea.

" Huku mbele tunapokwenda matumizi ya tehama yatakuwa makubwa kutokana na  Sayansi na Teknolojia  hasa kwa upande wa Mawasiliano.

"tunakwenda kufungua milango ya masoko na mauzo kwa wajasirimali kuuza biashara zao popote," ameaema.

Ameongeza kuwa hiyo ni  fursa hapa nchini kwa wenye viwanda na watu wetu wajasiriamali kutumia duka mtsndaoni popote alipo.


"Tunataka kuwa na posta ya kidigitali, tunajikita na huduma nyingine tumenunua magari matano na tutaongeza mengine ili kuweza kusafirisha kwa wakati.

Aidha ameeleza kuwa wanakuja na sheria ambayo inaenda kusimamia taarifa binafisi.

Kwa upande wake  Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo amesema kuwa tukio hilo linaimarisha ushirikiano hilo ni jambo jema  linaelekeza watu wafanye kazi kwa pamoja.

Kwa upande waletu mnatusadia kazi yetu mlichokufanya mnatutafutia biashara na inatoa fursa hadi sasa tafiti zinaonyesha kuwa hatujatumia mitandao kwa masuala ya kiuchumi

"Hapa tunaenda kunganisha wafanyabiashara na makapuni, mtu anaweza akawa na mambo makubwa bila kuwa na kibanda.," amesema Prof. Kitila.

No comments:

Post a Comment

Pages