Balozi wa Italia hapa nchini, Marco Lombard, akisalimiana na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka, alipowasili Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Saaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu Ndaki ya Dar es Salaam, Prof. Honest Ngowi, akitoa taarifa ya chuo hicho kwa Balozi wa Italia hapa nchini, Marco Lombard.Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka, akizungumza na Balozi wa Italia hapa nchini, Marco Lombard (katikati) alipotembelea chuo hicho.
Dar es Salaam, Tanzania
CHUO Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam washirikiana na serikali ya Italia katika kukuza vijana wenye weredi katika biashara na Ujasiriamali hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Makamu Mkuu Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka amesema chimbuko la ziara hii ni pamoja na mpango mkakati wa Chuo Kikuu Mzumbe kushirikiana na taasisi mbalimbali za nje na ndani ya Tanzania.
Kwa upande wa Italia, Chuo Kikuu Mzumbe kina makubaliano ya ushirikiano na Chuo Kikuu cha Catholic University of Milan. Kati ya mambo makubwa katika ushirikiano huu ni mpango wa kushirikiana katika kufundisha programu mpya ya masomo kwa ngazi ya uzamili katika eneo la usimamizi wa biashara katika ujasiriamali tumizi (Masters of Business Administartion – MBA - in Impact Entrepreneurship) siku za karibuni.
Hii ni programu inayolenga kupokea na kufundisha wajasiriamali ambao tayari wana biashara wanazotaka kuendeleza au wenye mawazo ya biashara wanayotaka
kutekeleza kwa vitendo wakati wakiwa chuoni na baada ya kuhitimu. Maandalizi ya kuanza programu hii yako mbioni. Lengo ni kuzalisha wajasiriamali watakaojiajiri na
kuajiri wengine.
Hii ni programu inayolenga kupokea na kufundisha wajasiriamali ambao tayari wana biashara wanazotaka kuendeleza au wenye mawazo ya biashara wanayotaka
kutekeleza kwa vitendo wakati wakiwa chuoni na baada ya kuhitimu. Maandalizi ya kuanza programu hii yako mbioni. Lengo ni kuzalisha wajasiriamali watakaojiajiri na
kuajiri wengine.
"Sisi Kama Chuo katika mpango mkakati tuna lengo la kupanua huduma hasa ushirikiano na vyuo vikuu vya ndani ya nchi, vyuo vya ukanda wa Afrika Masharikia, Afrika na nje ya bara la Afrika, na kwasasa tupo katika mazungumzo na Chuo cha Milan kilichopo Itali ili kuweza kuendesha program za pamoja."
Nasisi tunatamani vijana wetu wanaohitimu katika vyuo vikuu hapa nchini wawe wanauwezo wa kuazisha biashara, wa kuwa na miradi ya kijasiriamali ambayo itakuwa inatoa bidhaa zenye Ubora.
Amesema kupitia balozi wa Italia hapa nchini anaimani ya kuunganishwa na vyuo vingine vya nchini Italia ili kuweza kufanya mambo mengi kwa pamoja.
Ushirikiano huo utakuwa katika kuandika miradi ya utafiti na maendeleo ya jamii pamoja na vyuo hivyo na kuitekeleza nchini Tanzania na nchi nyingine.
si za elimu ya juu hapa nchini wanaweza kutoa elimu na kuwapa ujasili wa kufanya biashara na wadau wa kimataifa waliopo nchini Itali.
Amesema suala la kuongeza tija katika wahitimu wa Vyuo vikuu hapa nchini ni la Kiserikali kwani Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikifanya kazi kubwa sana katika kutoa elimu ya ujasiliamali kwa kila kada inayofundishwa hapa nchini.
Prof. Kusiluka amesema kuwa kila chuo kwa sasa hivi vinaboresha elimu kwa kufundisha ubunifu, ujasiriamali ili vijana wanaotoka wawe na mtizamo chanya hasa kwakuweza kujiajiri wenyewe na wawe na ujasili wa kuamini kwamba wao wanaweza kuwa wafanyabiashara wakubwa.
Amesema kuwa wahitimu wa vyuo vikuu hapa nchini ni wako vizuri na wanauwezo wa kufanya kazi vizuri kwahiyo amewatoa wasiwasi wahitimu wa hapa nchini kwani hata wakienda kwenye mashindano na vyuo vingine wanashindana vizuri na kuibuka videdea.
No comments:
Post a Comment